baba glory
JF-Expert Member
- Jan 22, 2016
- 292
- 213
Mie nilisahau vya kwangu kwenye daladala tangu 23/08/2015 Jana 8/05/2017 nimevipata yaani kama muujiza asee
NMEJIONGEZA BOSS
Waliopotelewa na vyeti vya taaluma wanapoomba kazi serikalini
Ndugu Katika mamlaka ya ajira Tanzania. Kutokana natangazo la hivi karibuni linalo eleza mambo ya kuzingatia Mimi ni Hemed A. Kavumo mmoja wa watu waliopotelewa na cheti cha form four na nimefanya taratibu zote na Necta na wakadai wameshatuma taarifa zangu tume ya ajira, tatizo ni kwamba sinahakika kua taarifa hizo zimewafikia tume ya ajira.
Wakati wa kuomba kazi kwa walio potelewa na vyeti napenda kuuliza maswali ya fuatayo.
Mtu aliye potelewa na cheti nakuripoti necta na akaambiwa taarifa zake zitatumwa nivipi atajua kama taarifa zake zakupotelewa na cheti zimewafikia tume ya ajira pindi anapo omba kazi?
Pili ni nanma gani tume ya ajira itafahamu kuwa mtu flani amepotelewa na cheti na sio kuwa hakutimiza vigezo au viambatanisho pindi anapoomba kazi serikalini?
Ushauri wangu ni kwamba aliyepotelewa na cheti na kutoa taarifa kwenye mamlaka husika na taarifa zake kutumwa mamlaka ya ajira apewe majibu kua taarifa zake zakupotelewa na cheti zimefika tume ya ajira na anapoomba kazi aandike barua kueleza kua taarifa za kupotelewa na cheti husika zimeshaifikia tume ya ajira ili kuepusha usumbufu na kuwezesha tume ya ajira ihakiki taarifa hizo.
Ahsante.
Jibu.
Tumepokea maswali yako, awali ya yote nikupe pole kwa kupotelewa na cheti cha kidato cha nne, Aidha ni kweli kwamba baadhi ya watu waliopotelewa na vyeti vya kidato cha nne na sita wanapoenda kuripoti Baraza la Mitihani (NECTA) juu ya upotevu wa vyeti vyao na wakaomba taarifa za kupoteza vyeti vyao zitumwe Sekretarieti ya Ajira utaratibu huo huwa unafanyika.
A) Kama ulipoteza cheti ukaripoti NECTA na ukawaomba taarifa zako wazitume Sekretarieti ya Ajira ili kufahamu unapaswa kuwasiliana na Sekretarieti ya ajira ili kuulizia kama jina lako limefika(unaweza kupiga simu kwa namba hii 0687 624975 au tuma ujumbe kwenye ukurasa wetu wa facebook www.facebook.com/sekretarieti ajiara). Pia unapoitwa kwenye usaili siku ya usaili kabla ya kufanya usaili ni vyema ukauliza ili jina lako liangaliwe kwenye orodha yetu tuliyoipata kutoka NECTA kujiridhisha kabla hujaingia kwenye usaili.
B) Sekretarieti ya ajira itafahamu kuwa mtu fulani amepotelewa cheti kwa kupata taarifa au jina kutoka mamlaka husika inayotoa cheti baada ya aliyepoteza cheti kutoa taarifa na kuomba jina lake litumwe sekretarieti ya ajira kama nilivyoeleza hapo awali.
C) Ushauri wako umepokelewa lakini pia unakumbushwa kufuata maelekezo yaliyopo katika maelezo ya awali katika jibu la kipengele (a) ili kujiepushia usumbufu usiokuwa na lazima ikiwemo kupunguza gharama.
eh eh boss mi JF toka mwaka 2011 kama degree ya udaktari..shukrani kwa kudelete folder la kikinjanjaIlibidi uweke maelezo mubashara namna hii ili tusikuweke
kwenye kundi la makanjanja. Kwa sasa nina kufuta kwenye "kishoka kanjanja folder"
eh eh boss mi JF toka mwaka 2011 kama degree ya udaktari..shukrani kwa kudelete folder la kikinjanja
Namba nnazo koz nna soft copy...najiandaa niende Polisi soon kituo nilifuatilia sema so unajua Mbagala...kikubwa kupata jibu linaloeleweka....vp swala LA uhakiki wakitaka original haiwezi athiri? Nipo kazini ila ni sekta binafsi...ila napenda kua safe side...its frustrating...ila shukran kwa ushauri
sio rahisi kuvipata.demand ya vyeti halisi kutoka kwa wenye vyeti feki ni kubwa
Hatakiwi kutulia baada ya hapo,anatakiwa kwenda hizo shule alizosoma ili kapata barua ya uthubitisho kuwa alisoma na kuhutimu shule hizo ambazo zitatumika Necta kapata matokeo yako in case mwajiri atataka kapata uhakika wa taarifa zake kuhusu vyeti.Lakini si ulishahakikiwa? Au ulikuwa hujapata ajira? Kama ndivyo basi toa taarifa polisi ili upate 'loss report' halafu utangaze kwenye gazeti la SERIKALI mwisho, chukua page ya gazeti iliyotoa hiyo taarifa then hifadhi hizo docs mbili, tulia!