NMB yaipa serikali gawio la bilioni 7.9 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NMB yaipa serikali gawio la bilioni 7.9

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kevin.A, Jun 12, 2012.

 1. K

  Kevin.A Member

  #1
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa kwa niaba ya serikali amepokea sh 7.9 bilioni kutoka benki ya NMB ikiwa ni gawio la serikali kwa mwaka 2011 kama ilivoidhinishwa katika mkutano wake mkuu uliofanyika Juni 2, 2012.Gawio hilo lilitokana na serikali kumiliki asilimia 31.8 ya hisa katika benki ya NMB.

  Akizungumza baada ya kupokea hundi hiyo jijini Dar es Salaam Dk. Mgimwa alisema, amefurahishwa na benki ya NMB kwa utendaji wake kwa kuwa mwaka 2010 iliweza kutoa sh bilioni 5.7 "Benki ya NMB inaonyesha dalili nzuri ya utendaji wake kwa kuwa ongezeko hili la mwaka 2011 la sh bilioni 7.9 kwa serikali ni ongezeko zuri na fedha hii iliyotolewa na NMB Imeweza kuichangia Serikali baada ya kupata faida kwa kuwa ni nyingi sana na itasaidia kuwalipa wafanyakazi wengi " alisema Dk.Mgimwa"

  Aidha, aliipongez NMB katika juhudi zake za kuisaidia serikali kupitia shughuli mbalimbali za kupambana na umasikini na kuboresha maisha ya wananchi wenye mahitaji. Alisema anathamini mchango wa NMB katika ukusanyaji wa kodi unaofanywa kupitia matawi yake yaliyosambaa Tanzania nzimai.

  Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa NMB, Bw. Mark Wiessing alisema NMB itaendelea kuleta huduma nafuu za kifedha kwa jamii ya kitanzania katika maeneo yote ya vijijini na mijini "NMB imeweza kufikia wateja wake nchi nzima,pia imeweza kulipa kodi kwa serikali,ndio maana NMB ni benki bora kwa Tanzania

  Tukio hilo muhimu lilishuhudiwa na manaibu wawili wa wizara ya Fedha na Uchumi, Katibu mkuu wa wizara ya fedha na manaibu wake watatu, mweka hazina mkuu, wakuu wa wizara zingine pamoja na wafanyakazi wa NMB.


  Source: Michuzi

  Swali:
  Je, Serikali ina chombo cha kufuatilia mapato halisi ya hii Bank?Kwangu mimi nahisi kama hili gawio ni dogo sana kwa serikali yenye hisa 31.8 kwenye NMB! Hainingii akilini kwa Waziri kuchekele na kutoa pongezi....
   
 2. i

  isotope JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 2,404
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Bil 7.9 tu, halafu anachekelea kama zuzu, dah!
   
 3. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,318
  Likes Received: 609
  Trophy Points: 280
  Kama NMB inatoa gawio linalokaribiana na kiasi tulichopokea kwa kuiuza NBC, bado tunaweza kushawishiwa kuwa kulikuwa na ulazima wa kuiuza banki ile?
   
 4. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,318
  Likes Received: 609
  Trophy Points: 280
  Unajua NBC iliuzwa kwa kiasi gani?
   
 5. Atukilia

  Atukilia JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 643
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mkuu angalia kwenye soko la hisa la DSM bei ya hisa za sekta ya kibenki ni shs ngapi, halafu angalia kwenye kikao cha mwaka wenye bodi ilipendekeza shs ngapi kama gawio. kumbuka wanahitaji fedha kupanuka na kuwekeza kwenye teknolojia
   
 6. p

  petrol JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 322
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Ingeuzwa kama serikali ilivyokuwa imepanga hiyo miaka ya nyuma, haya matunda tungepata? pengine wakati umefika kuangalia jinsi serikali inavyoweza kurejesha ubia wake kwenye maeneo nyeti kibishara na kihuduma (strategic areas)
   
 7. F

  Fernandes Rodri JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 405
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Bilioni 15
   
 8. t

  tara Senior Member

  #8
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Anachekelea jinsi itakavyotumika.....
   
 9. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #9
  Jun 12, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Hapo Lazima JK anafutafuta passport yake kwani hela ikipatikana lazima Asafiri kwi! kwi! kwi! kwi! aha
   
 10. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,318
  Likes Received: 609
  Trophy Points: 280
  And you can get that amount from dividends in 2 years? I know that by that time the value of 15 bn isn't the same today, but we were surely cheated somewhere, and I still believe that there was no gain in selling NBC.
   
 11. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #11
  Jun 12, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Tanzania has got no leaders but people with "dehydrated mind" who tries to lead others!! What do you expect in such kind of leadership guys? Ever since independence, nothing hopeful can be demonstrated as our pride. Everything is in slogan even sensitive matters. In such a situation, I dare to profesy that, under the leadership we have recently, we wont go anywhere economically. Think about "coward learders"
   
 12. m

  muta jr Member

  #12
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  Bravo nmb
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Jun 12, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  kuna mtu anaweza sema hili gawio kwa hisa moja ni kiasi gani?
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Jun 12, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  na je nmb inatoa gawio kila mwaka?
   
 15. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #15
  Jun 12, 2012
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,960
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 180
  Kwenye kikao cha bajeti kilichoanza leo, tunataka waziri wa fedha atueleze serikali inategemea kupata shilingi ngapi kutoka hisa za serikali ndani ya makapuni kama:- NBC Sigara TBL NMB Twiga cement Simba cement Mbeya cement Airtel N.k. Pia tunataka serikali itupe hesabu tunayopata kutoka makampuni yanayomilikiwa na serikali kwa asimia 100% kama:- Tume ya mawasiliano Tanapa Insurance Supervisory Authority TBS Wakala wa majengo Bandari Benki kuu Benki ya posta Benki ya rasilimali Mamlaka ya viwanja vya ndege Soko la hisa RITA EWURA TRA SUMATRA BRELA N.k. Tunataka serikali itueleze kwa muda wa miaka 10 iliyopita ilipokea kiasi gani cha fedha kutoka kila kampuni na zilitumika vipi.
   
 16. B

  Bob G JF Bronze Member

  #16
  Jun 12, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nani wakujua mapato halisi? Tuliambiwa na Mkapa hakuna mtanzania mwenye uwezo wa kuongoza NMB
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Jun 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ilipokuwa 100 kwa 100 "mali ya umma" ilikuwa mpaka yenyewe isaidiwe. Halafu bado mijitu inashikilia kusifia mfumo mbovu wa "mali za umma" uliokuwa hauna faida yoyote kwa Taifa.
   
 18. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,721
  Likes Received: 1,630
  Trophy Points: 280
  hizi hela wanawapa za nini bora wangezipeleka kwa wateja wake wanaosota na mikopo bila mafanikio.
   
Loading...