NMB kunani, nimeambiwa mikopo imesitishwa?

NMB kunani, nimeambiwa mikopo imesitishwa?

Ulika

Member
Joined
May 1, 2013
Posts
13
Reaction score
3
Najiuliza sana ila sipati jibu la hii serikali ina mpango gani na raia. Leo imekataza semina, kushusha madaraja na kustopisha mpaka ukaguzi hewa kwa wafanyakazi hewa upite hususani kwa waalimu na wafanyakazi wa serikali.

Nimekaa nikawaza nikaona sio kesi ngoja nifanye biashara nijiongezee kipato, si nikagonga hodi benki ya NMB ile naonana tu na afisa mikopo ananambia mikopo imesitishwa.

Nikamuuliza kwa mshangao, "kwanini"? Naye akaniuliza, "kwani ulishawahi kukopa?" Nikamjibu bado ndo first time akasema basi subiri mpaka Januari. Nikasepa bila kuagana, naona kama program yangu imefeli.
 
Najiuliza sana ila sipati jibu na hii serikali inampango gani na raia leo imekataza semina, kushusha madaraja na kustopisha mpkaka ukaguzi hewa kwa wafanyakazi hewa upite hususani kwa waalimuna wafanyakazi wa serikali...nimekaa nikawaza nikaona sio kesi ngoja nifanye biashara nijiongezee kipato si nikagonga hodi benki ya NMB ile naonana tu na afsa mikopo ananambia mikopo imesitishwa ....nikamuuliza kwa mshangao kwa nini? nae akaniuliza kwani ulisha wahi kukopa? nikamjibu bado ndo first time akasema basi subiri mpaka januari....nikasepa bila kuagana naona kama program yangu imefeli.
c nmb tu kazi ipo....
 
Hakuna mikopo halafu tunahimizwa na kuambiwa tujiajiri, sijui kama wako timamu hawa.
 
Namba inasomeka poteeeeeee! Chaguo letu wanyeweeee! Tumeipenda wenyeweeeee, tuvimbe natupasukeeeeee!
MWAKA HUU TUTAISOMA NAMBA EEEEEEEEEH! CCM MBELE KWA MBELE! Huo wimbo unaujua unamaana gani kimaudhui? Ndo ilan inayotekelezwa sasa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom