NMB branch ya Mlimani City badilikeni

Lokii

JF-Expert Member
Sep 23, 2016
533
1,000
Wasaalam wanaJF,

Leo nilienda bank ya NMB branch ya pale mlimani city ku-deposit ila nilivyoingia ndani nilishangaa kuona hiyo queue ya kwenda TELLER jinsi ilivyo ndefu afu watu wamesimama, kiukweli ilibaki kidogo nikate shauri ya kuendelea na hilo zoezi mana nilijiuliza mda nitakaochukua mpaka kufika kwa teller afu kibaya zaidi nikiwa nimesimama

Bank nyingine pale mlimani city(CRDB na EXIM) wameweka viti kwa wanaoenda kwenye teller yaani mtu unapanga foleni ukiwa umekaa kwenye kiti sasa nashangaa nyie NMB sijui mmeshindwa nini wakati pale wanaposimama watu kupanga foleni kuna nafasi ya kutosha kabisa kama mngetaka kuweka viti, kwanini msiige hili kutoka kwa hao wenzenu? mbona ni kama bado mko kwenye ujima??

mkiishamaliza kutuwekea viti msisahau na QMS(Queue Management System) kama ilivyo pale CRDB hii itafaa sana kwasabu kuna mijitu ilikua inapiga anti-queue bila kujali kama kila mtu alikua na haraka sasa hii QMS itawastaarabisha sana watu wa aina hiyo na kufanya ile kanuni ya FIFO(first in first out) kuzingatiwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom