Nlimwomba Mke wangu anilishe Limbwata...

Sodoku

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2016
Posts
1,277
Reaction score
2,933
Nimelazimika kuandika hili kutokana na hali ambayo wakati mwingine nakutana nayo kutoka kwa jamaa zangu. ni miaka kadhaa sasa toka nimeoa na nimekutana na changamoto kadhaa mpaka kufikia hatua ya kusema liwalo na liwe.

nlikuwa na marafik kabla ya ndoa na baada ya ndoa. popote pale wanapokusanyika binadamu kunakuwa na changamoto zake. ukiwa ofisini ukawa unafanya kazi kwa bidii na unafuata sheria na taratibu zote kuna watu watakuchukia na kukuona unajipendekeza au una shida sana hivyo unaogopa kuvukuzwa kazi. hali kadhalika ......

kwa sisi ambao tumeamua kuwapenda wake zetu wanasema tumerogezewa au tumerogwa. ugomvi wangu ni jamaa zangu ni kuwa pamoja na wao kuwa wameoa ila ikifika saa 3 usiku mi naaga kuwa lazima nirudi home.wakati wao ndo kwanza kumekucha na wanawapigia simu wengine walio majumbani waje kuanza/kumalizia weekend. wanashangaa wakinambia twende sehemu ghafla, nawaambia sijamwaga wife. wao wanaona huo ni ufala. au nikiwa nao sehemu wife akipiga simu kuulizia nikimweleza wao wanashangaa sana. jamaa wamefikia hatua wamenitenga na hawataki tukae pamoja. siwalaumu labda nawabore kwa kuwa wao huwa wakiwa maeneo hayo hawapigiwi simu na wake zao na ikitokea wamepigiwa wanaweza wasipokee au mtu akawa mkali sana akifoka.

kiuhalisia mimi kama nimepewa limbwata basi la namna hii nimelipenda na nashauri hata wewe mwingine kama una family yako mwambie mkeo akuwekee limbwata. haiwezekani sisi wanaume tunaenda kunywa na kurudi home saa nane au kumi alfajiri kwa kuamini tu mwanamke hana haki ya kuuliza as long as anakula na anavaa.

imani ya kuwa kuomba ruhusa kwa mkeo ni udhaifu au ni kuonesha umetekwa ni moja ya imani mbovu sana. ukishakuwa na ndoa wewe tena hujimiliki. mwili wako na maamuzi yako si ya peke yako. si ajabu akakwambia hataki kuona umevaa nguo flan na ukalazimika kuvua. haya mambo wanaume tusidhani uana ume ni kuwa mbabe kwa mkeo. hayo ni maisha ya kizamani sana. miaka hii hatutangazi ubabe kwa wake zetu. wake ni marafiki,wapenzi,ndugu n.k

wacha mimi niendelee kula limbwata la mke wangu na as long as nlimwomba kabla sijamwoa kuwa niwekee limbwata ( figuratively ) sijuti kabisa. na ninyi ambao ni wanaume hasa endeleeni kuonesha uana ume wenu.
 
Uko sahihi kiongozi wala hujakosea..
 
Mkuu, mambo ya giza utayaombaje au kuyaonaje kirahisi hivyo? Hufanyika gizani. Ha ha ha ha ha ha
 
Mkuu kwa maoni yangu hayo uliyo ya bainisha kama limbwata wala sio 'limbwata' kwa mtizamo wangu ulichokielezea ktk mada ndo hasa inavyotakiwa watu wakae na wake zao na kwa hao marafiki zako naona ni mitindo yao tu ya maisha , mfano hivi inakuwaje unarudi kwako kila siku usiku wa manane na umeoa

Hayo unayofanya ndo kuheshimiana ktk ndoa na hasa kama uhusiano una afya mengine ni ubabe wa kiume na mapokeo tu

Lkn leta mrejesho labda mkeo anakufokea mbele za watu, anafukuza ndugu zako lkn ndugu zake wamejazana kwenu au anarudishwa na 'jamaa' usiku mkubwa kalewa nawe wa kumfungulia mlango hapo ndo tutajiuliza dhana nzima ya 'limbwata' lkn kwa ulichokiandika kwa mtizamo wangu huo ni ustaarabu wa kawaida tu kwenye ndoa
 
Nimelazimika kuandika hili kutokana na hali ambayo wakati mwingine nakutana nayo kutoka kwa jamaa zangu. ni miaka kadhaa sasa toka nimeoa na nimekutana na changamoto kadhaa mpaka kufikia hatua ya kusema liwalo na liwe.

nlikuwa na marafik kabla ya ndoa na baada ya ndoa. popote pale wanapokusanyika binadamu kunakuwa na changamoto zake. ukiwa ofisini ukawa unafanya kazi kwa bidii na unafuata sheria na taratibu zote kuna watu watakuchukia na kukuona unajipendekeza au una shida sana hivyo unaogopa kuvukuzwa kazi. hali kadhalika ......

kwa sisi ambao tumeamua kuwapenda wake zetu wanasema tumerogezewa au tumerogwa. ugomvi wangu ni jamaa zangu ni kuwa pamoja na wao kuwa wameoa ila ikifika saa 3 usiku mi naaga kuwa lazima nirudi home.wakati wao ndo kwanza kumekucha na wanawapigia simu wengine walio majumbani waje kuanza/kumalizia weekend. wanashangaa wakinambia twende sehemu ghafla, nawaambia sijamwaga wife. wao wanaona huo ni ufala. au nikiwa nao sehemu wife akipiga simu kuulizia nikimweleza wao wanashangaa sana. jamaa wamefikia hatua wamenitenga na hawataki tukae pamoja. siwalaumu labda nawabore kwa kuwa wao huwa wakiwa maeneo hayo hawapigiwi simu na wake zao na ikitokea wamepigiwa wanaweza wasipokee au mtu akawa mkali sana akifoka.

kiuhalisia mimi kama nimepewa limbwata basi la namna hii nimelipenda na nashauri hata wewe mwingine kama una family yako mwambie mkeo akuwekee limbwata. haiwezekani sisi wanaume tunaenda kunywa na kurudi home saa nane au kumi alfajiri kwa kuamini tu mwanamke hana haki ya kuuliza as long as anakula na anavaa.

imani ya kuwa kuomba ruhusa kwa mkeo ni udhaifu au ni kuonesha umetekwa ni moja ya imani mbovu sana. ukishakuwa na ndoa wewe tena hujimiliki. mwili wako na maamuzi yako si ya peke yako. si ajabu akakwambia hataki kuona umevaa nguo flan na ukalazimika kuvua. haya mambo wanaume tusidhani uana ume ni kuwa mbabe kwa mkeo. hayo ni maisha ya kizamani sana. miaka hii hatutangazi ubabe kwa wake zetu. wake ni marafiki,wapenzi,ndugu n.k

wacha mimi niendelee kula limbwata la mke wangu na as long as nlimwomba kabla sijamwoa kuwa niwekee limbwata ( figuratively ) sijuti kabisa. na ninyi ambao ni wanaume hasa endeleeni kuonesha uana ume wenu.

Yaani leo maisha yamebadilika hivi hadi Mbwa anamuomba Chatu amuue na ammeze? Sasa naanza kuamini kuwa ukistaajabu ya Musa basi utayaona ya Firauni.
 
Kaza baba.. Unafanya ya maana, mara nyingi company ndio huwa zinapoteza watu.
 
kuna jamaa anaitwa GuDume alikuwa anatafuta mke nadhan ana sifa hizo
pia yupo @gagadudu
Jaman kama kuna mwanaume anayepatikana Wa namna hii,nipo teyari ata ndoa ya mkeka.

Au kaka huna mpango wa kuongeza mke wa pili?
 
kiukweli mke wangu hajawah kunivunjia heshima. ana niheshimu na mambo mengine ni ya kawaida tu. sema jamaa zangu wanahisi kuwa ntakuwa nmewekewa limbwata sababu ya hayo nliyoeleza. kuna jamaa ikifika ijumaa anarudi home kwake saa kumi au 11 asubuh. then akija kuondoka tena jumapili saa 10 /11 asubuh ni mmoja ya majamaa zangu. sasa napomwambia mimi muda flan siwez toka huwa anatingisha kichwa kwa masikitiko. na sasa nimeambiwa wanakaa wanasema inabidi waangalie namna gan ya kunikwambua toka kwenye limbwata.wanasema haiwezekani mwanaume unaomba ruhusa ya kutoka. haiwezekani unasema unawah kurudi home unawaacha wanaume wenzio bar. au jumamosi, jumapili unashinda home au unakuwa na family somewhere kama vile huna kampani ya wanaume.
 
OTE="Sodoku, post: 23809386, member: 351185"]kuna jamaa anaitwa GuDume alikuwa anatafuta mke nadhan ana sifa hizo
pia yupo @gagadudu[/QUOTE]
Majina yao tu hata na billion siwataki
 
Back
Top Bottom