Cassablanca
JF-Expert Member
- Jan 24, 2018
- 324
- 590
Wafanyakazi wakisafisha makombora aina ya 'Shaheen' kabla ya paredi ya kijeshi, Islamabad, Pakistani, March
(Picha by Careen Ferouz/Reuter)
Wachambuzi wa mambo wanasema North Korea yataka mfumo wa makubaliano yake na US uwe kama ule uliofanywa kwa Pakistan, nchi masikini iliyojitoa muhanga kufanya tafiti za utengenezaji wa silaha za nyuklia na hadi sasa wanazimiliki.
Pakistani walianza programu yao ya silaha za nyuklia miaka ya 1970s kwa malengo ya kuwaogofya adui wao mwenye nguvu kubwa India. Zulfikar Ali Bhutto, mwanasiasa aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Pakistan, alisema kuwa kama India watatengeneza bomu (fulani), basi na wao (wapakistani) watakuwa tayari kula nyasi na majani mpaka watengeneze bomu mfano wake. Mnamo 1998 mchana kweupeee Pakistani ikafanya majaribio mfululizo ya silaha za nyuklia. Mwanasayansi mkuu akasema "Ashukuriwe Mungu" na akabonyeza kitufe kilichosababisha mlima kutetema kutokana na mlipuko mkubwa.
Mwaka 2016 Pakistani imeripotiwa kuwa na vichwa vya nyuklia 130-140.
NK haitaki kufuata mfumo wa Libya, ambapo baada ya Gadafi kukabidhi programu yake ya silaha za nyuklia kwa US 2003/4 baadae 2011 ilivamiwa na US na washirika wake hatimaye utawala wake kuangushwa.
Pia NK haitaki kufuata njia ya Iraq ambayo baada ya Iraq kutangaza kuachana na programu yake ya silaha za maangamizi na kuwaita wataalamu kuhakiki LAKINI ilivamiwa na utawala wake kuangushwa.
North Korea Wants to End up Like Pakistan, Not Libya