Njooni mtusaidie - Iraq kwa Marekani

Njooni mtusaidie - Iraq kwa Marekani

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
33,574
Reaction score
53,605
19 Juni, 2014 - Saa 00:30 GMT

140505050225_cn_east_pacific_rescue_512x288_usairforce_nocredit.jpg

Majeshi ya angani ya MArekani kutumwa Iraq



Iraq imeomba rasmi usaidizi wa Marekani kushambulia kwa ndege wapiganaji wa kiislamu walioteka miji kadhaa nchini humo wiki hii.
"Tumepokea ombi kutoka kwa serikali ya Iraq kutumia ndege zetu huko,'' alithibitisha kamanda mkuu wa jeshi la Marekani Jenerali Martin Dempsey mbele ya baraza la senate.
ISIS waendeleza harakati zao

140617161700_iraq_isis_512x288_bbc_nocredit.jpg

wapiganaji wa ISIS wameilemea serikali ya Iraq


Awali wapiganaji hao wa madhehebu ya Sunni walishambulia kiwanda kikubwa zaidi cha kusafishia mafuta nchini Iraq katika mji wa Baiji kaskazini mwa Baghdad.

Katika taarifa yake kwa taifa, waziri mkuu Nouri AL Maliki alitoa wito kwa raia wa Iraq waungane dhidi ya wanamgambo.

Vikosi vya jeshi vinajitahidi kuwakabili na kuwasukuma nje wanamgambo wa ISIS pamoja na washirika wao wa Ki-sunni kutoka mikoa ya Diyala na Salahuddin baada ya waasi hao kuteka mji wa Mosul wiki iliyopita.

Obama ataka kuisaidia Iraq

Na hapo Jumatano, rais Barack Obama alifanya kikao cha dharura na baraza la Congress kujadili mzozo wa Iraq.

Duru za ikulu ya White house zinasema kuwa Bwana Obama ''amependekeza kuongezwa juhudi zetu nchini Iraq na kusaidia majeshi ya serikali hiyo katika kukabiliana na wanamgambo wa ISIS ikiwemo uwezekano wa kuongeza usaidizi wa kiusalama''.
Baadhi wanapinga

Lakini kabla ya kufanyika mkutano huo, kinara wa baraza la Senatae wa Marekani Harry Reid, kutoka chama cha Demokrats alisema kuwa hakubaliani kamwe na wazo la kuihusisha Marekani katika ''vita vya ndani vya Iraq''.

Marekani imekuwa katika ubishi mkubwa katika mabunge ya Senate na Congress juu ya kuondolewa majeshi yao ndani ya Iraq na Afghanistan.


Njooni mtusaidie - Iraq kwa Marekani - BBC Swahili - Habari

 
Kuna uzembe ulifanyika toka mwanzo

So as to Kenya
 
Kuwasaidia ili kuwa si kumuondoa saddam madarakani bali kumsaidia kubadili baadhi ya mambo ..... aya ya sasa yasingetokea wasisahau libya pia wao ndio wamepachafua wakapasafishe
 
Obama hawezi kumsaidia kwani yeye ndo kawatuma wale jamaa,ndo maana wamesema hawatoi msaada mpaka waziri mkuu aachie ngazi.
 
Kuwasaidia ili kuwa si kumuondoa saddam madarakani bali kumsaidia kubadili baadhi ya mambo ..... aya ya sasa yasingetokea wasisahau libya pia wao ndio wamepachafua wakapasafishe

Suala la Iraq ni mfano mmoja tu, ni vema International community ikashughulikia tatizo la islamists duniani kote, hawa ni hatari sana,nchi zifutazo zisipokabili hawa wanaojiita wako karibu zaidi na mungu itakuwa ni majanga 1, ZANZIBAR 2. AFGHANISTAN, 3 NIGERIA, 4 KENYA, 5 MALI, 6 ARUSHA(waliponzwa tu). Nchi za kiislamu na za kiarabu wakatazeni hao ndugu zenu wanaoudharirisha uislamu kwa kisingizio cha kudai haki za kisiasa. Ingawa waarabu by nature ni wakatili sana lakini wanaweza kuiga falsafa za kikristu ambazo zinahamasisha amani na upendo bila kulazimisha au kumwaga damu kuenforce hiyo amani, bila hivyo god will continue panishing you people if you will not change your cruel religious stands.
 
Obama hawezi kumsaidia kwani yeye ndie aliewatuma wale jamaa,ndo maana wamesema hawatoi msaada mpaka waziri mkuu aachie ngazi.


sure'
wale ni waasi wa Syria wameingia Iraq kwaajili ya kuindaa dola mpya itakayoivamia upya Syria na washirika wake
 
Hivi Iran hawezi kwenda kuokoa jahazi? Au jeshi lake ni la maonesho.
 
Arusha hakuna hii kitu mzee,
Alafu arusha sio nchi.
 
Back
Top Bottom