Njoo uwekeze kwenye biashara ya mafuta (Fuel) kwa laki 1 tu kama kima cha chini

Ndugu zangu tujitahidi kuwa wakweli kwa sasa biashara ya mafuta haelipi kabisa kwa watu wenye mitaji midogo kutokana na kodi na tozo mbalimbali kwenye bidhaa za petrol. Mashine za EFP zimeharibu sana TRA wanachukuwa full kodi, Services levy wanachuukuwa periodic report bado OSHA, EWURA, WMA, NEMC, TAPSOA , bika kusahau. Sheria ya mpya upakiaji mizigo imeongeza gharama za uchukuzi
 
Utapigwa hio 200M upate ukichaa wa ghafla!
 
Biashara ya mafuta imekuwa na ushindani sana , huu ushindani umrpunguza sana faida , unakuta ubaoni bei inasoma 2218 PMS , GO 2251 ukiengia ndani unapewa discount had I 150- 200|= kituo kinachojitahidi kuwa na mauzo mazuri kinauza Lita 300,000 kwa mwezi vituo vya kawaida vinauza Lita 150,000. Vingine vjnauza chini ya Lita 100,000/= profit margin per liter 70-120|= times mauzo then toa Upotevu was mafuta kwenye tanker lako kituoni (UST) then toa truck short madereva wanaeba mafuta wanayokubebea, then toa services kevy 0.03 ya mauzo yako then toa kodi ya pango / kituo cha mafuta sio less than 4M per months,then toa salary ya wafanyakazi, then toa OSHA Bills in more than 2M per year then toa NEMC fee, then toa EWURA licences fees then toa business licences fee , finally toa utakavyopigwa na manager wako. Hapo utaweza toa Gawio ka 10% kwa kila aliyewekeza?



 
Hivi bado hujang'amua kwamba huyu jamaa ni tapeli. Tena amekuja na mbinu ya kishamba kweli. Hamna biashara inayoweza ku guarantee faida ya namna hio duniani labda ya stocks and bonds ambayo ni ngumu sana kwa wasio na mitaji!
 
Haya maneno kwa sasa ni matamu kweli lakini ukijiunga baadaye yatakuwa machungu sana
 
Tangu nimepigwa pesa na yule mama Anajiita Bi.Ubwa wa NAMAINGO ahahah..sitakaa kutapeliwa kizembe namna hii.I believe in hard work ili kupata pesa.
"Ukiona unaitwa sanaa kwenye dili nwa watu wa design hii, basi jua ww ndio dili lenyewe"

Sitasahau huu msemo
 
Hii mbinu mnayotumia nyie watu wa biashara za mtandao (Q net, bitclub, Aliance n.k) tulishaishtukia kitambo, atakayepigwa ni kwa ujinga wake. AKILI KICHWANI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba nije nianze na laki 5, ila ombi langu kama kuna kibarua chochote ila sio chaofisini hata kama kitakuwa kinahitaji nguvu kidogo nipatiacho niwe kibarua vilevile mwekezaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi nondo ndio zinampeleka pangoni kabisa.
Maswali rahisi kama jina la kampuni ameshindwa kujibu.
 
Mambo Ni Moto na Jua linawaka sana siku hizi........mkuu nmekuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona hii no kama DECI!
 
Kuna point 2 zinanipa shida,
Moja ni kwanini mwanahisa anahusika na faida tu lakini hausiki na hasara.
Mbili...
Je biashara hii ikitokea hasara pesa ya kuwalipa wanahisa inatoka katika mfuko gani?
Na nyongeza ni kwamba ukokotozi wa mgawo wa wanahisa huwa unabase ktk faida iliyo ktk financial report. Sasa kama wanahisa hawaambiwi hasara, nyie kuna siku mtakosa cha kuwalipa wanahisa maana inamaanisha kuwa hapatakuwa na ukaguzi ktk fedha wala mahesabu ya kampuni.
Na nyongeza ni kuwa vp kuhusu isuarance ya mtaji??????????
Kama kampuni haina financial report haiwezi kujua km ina faida au hasara.

People be care this may be a scam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…