Njoo tujadili kuhusu: Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za AMD

the great wizard

JF-Expert Member
Dec 21, 2015
1,458
2,000
From chief mkwawa
"Computer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi."
Hapo juu waliongelea kuhusu vifaa vitumiavyo processor za intel tu sasa njooni hapa tuongelee kuhusu vifaa vitumiavyo processor za AMD
mimi sina experience na cpu za amd nimezoe sana kutumia computer za intel so nilitaka kubadilisha computer na ninataka nisitumie computer zitumianzo cpu za intel nataka cpu za AMD

nimeona cpu nyingi za amd but sielewi ipi itakuwa na nguvu kubwa kama labda cpu ya intel core i5 8600k zipo cpu ngingi za Amd kama
Athlon
Athlon 64 x2
Althlon 64
Althlon II
Phenom II
Sempron
Ryzen. Zen 1,Zen 2
etc
So kama unauzoefu wa vifaa hivi vya amd karibu hapa tueleweshane vizuri juu ya uchaguzi wa computer Zeyenye processor nzuri za AMD
 

VAN HEIST

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
1,432
2,000
ryzen 5 ina perfomance sawa na core i5 8600k zinapishana kwenye baadhi ya maeneo kwa mfano i5 hiyo ni "light" weight threads(zipo 6 na core zipo 6) ila kwa amd ni "heavy" weight threads (zipo 12 na core zipo 6) ila mara nyingi intel ni standalone ila kwa amd perfomance inategemea na uwepo wa external gpu

katika hiyo list yako zinazoweza kushindana na 8600k ni ryzen series hizo nyingine ni za kawaida

kwa ujumla unapotaka kununua pc inayotumia amd (sio amd peke yake) angalia kwenye idadi ya threads na cores (zaidi ni idadi ya thread), cache memory na TDP(thermal design power) pia uwezo wa kufanya kazi kama standalone au ikiwa na external gpu.

hii inajumuisha matoleo yote ya processor kwa mfano hiyo ryzen 5 kuna 1600X na 2400G ingawa zote ni ryzen lakini hazifanani kwenye specifications (mfano threads) kwa hiyo ni vyema kama utachagua processor kulingana na matumizi unayotaka.
 

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
24,034
2,000
kama alivyosema mdau hapo juu cpu za zamani za amd zote hazina maana zilikuwa zinakula umeme mwingi, single thread perfomance mbovu, hazina gpu za ndani etc

hizi cpu zao mpya za ryzen ndio nzuri zinacompete na intel kwa kula umeme kidogo na pia single thread perfomance wamejitahidi, japo intel anaongoza ila gape sasa hivi ni dogo.

Ryzen lineup
hili toleo la ryzen kwa sisi watumiaji wa kawaida kuna ryzen 3, 5 na 7 kama vile unavyosema i3/i5/i7 za intel

-ryzen 3 yenyewe ni ndogo inacompete na i3 ina core 4 na thread 4
-ryzen 5 ni ya kati kati ina core 4 au 6 na thread 8 au 12
-ryzen 7 yenyewe ni core 8 na thread 16

pia kwa wenye matumizi makubwa na workstation kuna threadripper ambayo inacompete na i7 zenye core nyingi, hii threadripper ina core 8 mpaka 16 na thread 16 mpaka 32

kwa ujumla angalia hii picha kuona lineup
Ryzen-Price-Chart.png


AMD APU
kikawaida cpu za AMD haziji na gpu ya ndani kabisa, hizo ryzen za juu nyingi hazina gpu, unaponunua desktop yake inabidi ununue na gpu separate. ila ipo lineup ya APU, hili ni jina la AMD linalomaanisha cpu zenye gpu, na mara Nyingi Apu za Amd huwa na nguvu kuliko gpu za intel.

lineup ya Apu za ryzen ni hii
-ryzen 3 2200g core 4 thread 4
-ryzen 5 2400g core 4 thread 8
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom