NJOMBE: Raia Wapigwa marufuku kula kitimoto

NJOMBE: Raia Wapigwa marufuku kula kitimoto

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,183
Reaction score
2,100
Ofisa Mifugo na Uvuvi wilayani humo, Aldo Mwapinga, alitoa amri hiyo kutokana na vifo vya nguruwe 21.

"Kata ya Tandala kumeripotiwa dalili za ugonjwa wa homa ya nguruwe kwa hiyo tunaendelea na jitihada za kuhakikisha tunashirikiana na watendaji kuanzia ngazi ya kata hadi vitongoji kutoa taarifa juu ya hali inavyoendelea," alisema.

Alisema: "Baada ya kupata taarifa hizi tumesimamisha zoezi la uchinjaji wa nguruwe katika kila eneo la kata ya Tandala, na pili kutoa nguruwe kuwapeleka kwenye maeneo mengine, pia tumezuia utoaji nguruwe kutoa zizi moja kwenda jengine kwa ajili ya kupandisha kwa jike," alisema Mwapinga.

Mwapinga, aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano pamoja na kutekeleza maagizo yote yanayotolewa na wataalamu wa mifugo ikiwamo kuacha kufukua nguruwe waliofukiwa baada ya kufa, kuwachinja na kwenda kuuza nyama hizo vilabuni nyakati za usiku.

"Nawaomba wananchi watupe ushirikiano kwa kutupa taarifa kila kifo kinachotokea, kuacha kufukua mizoga ili kuhakikisha jamii yetu inakua salama kwa kufuata maelekezo," alisema Mwapinga.

Alisema, inawezekana kuutokomeza ugonjwa wa homa ya nguruwe na kuwa historia katika maeneo yao.

Chanzo: Nipashe
 
Jmn kila muda huu mdudu anabebeshwa rundo la lawama na kuzingiziwa magonjwa. Yamilipuko mm Ni mtahalamu wa kuchinja nguruwe
 
halafu huko kunako hatari watu ndio wanajisomba sana kama kwenye K sijui binadamu wana nini aise ...
 
Vitu vyote vilivyokatazwa kwenye dini ya uislam vinamadhara ikiwemo pombe na kitimoto.
 
Back
Top Bottom