Huwa sielewi ni nini hasa faida ya njia hizo. Maeneo mengi utakuta zimegeuzwa maeneo ya biashara tofauti na kisudi lake. Hii ni pamoja na vituo vya daladala. Kuna haja ya kuingia gharama kujenga kitu ambacho hata hakina manufaa?
Faida ipo tena kubwa sana tu,ila tatizo mkuu ni sisi watanzania wenyewe,hatueleweki!hatujitambui. Vema na kosa machoni kwetu zinafanana tu. Yaani hata makaburini tunajenga tu,mtoni tunaishi bila shida tukifukuzwafukuzwa na mgambo tunachimba mkwala balaa! Sasa nani atusaidie?maana sote tunajua kabisa hizo ni njia.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.