Jayspeed
Senior Member
- Feb 23, 2014
- 156
- 168
Njia za kutimiza malengo yako:
Njia hizi zilisemwa na LEO BABAUTA mwandishi mashuhuri wa vitabu marekani na mmiliki wa blog ujilikanayo kwa jina la ZEN HABITS ila mimi nimezielezea kwa uelewa wangu na Mungu alivonijalia ..leo nitaanza na njia mbili halafu tutaendelea hivyo hivyo mpaka mwisho wa njia zote
1:CHUNGUZA MALENGO YAKO
Yachunguze malengo yako ulionayo kisha angalia ambalo unaweza kulifanikisha kwa urahisi ....
Unapochunguza malengo yako lazima utajua ndani ya malengo yako kuna lengo moja unalipenda zaidi kuliko mengine mfano malengo yako ni kuwa na gari, nyumba mke na watoto lakini ukichunguza kwa makini lazima katika vyote hivo kuna moja unapenda kulikamilisha haraka ...na hilo unalolipenda sana lichague kuwa la kuanza nalo na akili yako yote iwe inawaza kukamilisha lengo hilo hii itakusaidia kukamilisa lengo lako
LEO BABAUTA anasema " kujua lengo moja unalolipenda zaidi itasaidia kulifanyia kazi lengo lako vizuri zaidi..kufanya kitu ambacho unataka kitimie kweli utakikamilisha tu hata upitie changamoto nyingi.."
2: ANZA TARATIBU
Hata gari linapoanza kuondoka au treni au hata ndege haianzi na kuondoka kwa kasi tu lazima ianze taratibu kisha ichanganye na kushika mwendo...unapotaka kuanza lengo lako mfano una kiasi cha milioni tano usiwekeze zote anza taratibu usianzishe biashara kubwa Ambayo haitabakisha hela ya mengineyo hii itakuwia vigumu kuiendesha biashara yako ..jifunze kwenye hatua za mtoto mchanga kuanzia anaanza kukaa kisha kutambaa na kutembea
Wekeza mtaji ukizalisha ongeza mtaji wako kila unapofanya hesabu za mwisho wa mwaka au nusu mwaka....
Hakuna aliefanikiwa kwa haraka bila kuanza taratibu labda mali za urithi....
3 CHAGUA LENGO MOJA.
Watu wengi wanashindwa kukamilisha malengo yao kutokana na tamaa ya kukamilisha kila alichotaka kufanya ndani ya muda mfupi hapo ni ngumu sana. Fikiria tu hata Mungu hakuiumba dunia, wanyama na binadamu kwa siku moja. Katika malengo uliojiwekea kutimiza ndani ya mwaka huu kuna malengo yana umuhimu zaidi ya mengine hapa ndipo unapotakiwa kutoa kipaumbele kwenye lengo lenye umuhimu zaidi kuliko yote. Unapochagua lengo moja kwanza inakupa ari ya kukamilisha ili ufikie lengo lingine
Babauta anasema kuwa" huwezi kuwa na nguvu ya kuangalia mambo mawili ya umuhimu zaidi kwa wakati mmoja, hii itakusumbua sana utajikuta unakwama kila mwaka au mambo yanaenda taratibu zaidi ya ulivyotegemea"
Hii tunajifunza hata kwenye vitabu vya dini zetu kuwa kila jambo na wakati wake.
4:LIWEKE LENGO LAKO HADHARANI
Leo babauta anasema " usiweke lengo lako kwenye moyo tu wala kuandika mahali kisha kukaa kimya..shirikisha marafiki ndugu zako na ukianza kufanya kila hatua unayofikia washirikishe tena usisite kuwaambia ulipofika hata ukikwama kuwa wazi hii itakusaidia kupata mawazo mapya kila wakati"
Hii ipo sana hapa nchini ukikutana na mtu ukamuuliza lengo lako ni lipi mwaka huu anajiuma uma anabaki kusema ngoja utaona tu..
Kuficha lengo lako wakati mwingine unapishana na msaada kwa watu sababu watu hawajui unahitaji nini.. Wakati mwingine unapoweka wazi unapata msaada kwa watu uliowashirikisha lengo lako..
Unapoweka siri lengo lako wakati mwingine utakua unahitaji msaada ila kwakua umefanya siri utaanzaje kuomba msaada utasema msaada wa nini unahitaji?. Jifunze kuwa muwazi ili upate msaada kila unapohitaji
5: LIFURAHIE LENGO LAKO
Watu wengi huanza kufanya lengo lao vizuri lakini wanapofika katikati wanakutana na vikwazo vingi wanajikuta wanachukia walichokua wanakifanya.. Hata unapokutana na vikwazo vingi kiasi gani lifurahie lengo lako kwasababu unataka litimie.Mfano hayati baba wa taifa mwl. J.K.Nyerere angechukia harakati zake za kuutafuta uhuru wa nchi yetu labda leo tusingekua moja ya nchi yanye amani.. Mwlm alikutana na changamoto nyingi sana lakini alifurahia vikwazo sababu alkua anabuni mbinu nyingine mpya za kutafuta alichokua anakitaka na hatimae mwishoni alikipata.
6: CHAPISHA LENGO LAKO
Andika lengo lako mahali tena kwa maandishi makubwa..andika sehemu ambayo kila siku ukipita lazima ukutane na hiyo sehemu hii itakufanya kufanyia kazi ulichodhamiria
'' liweke lengo lako kwenye computer yako au hata kwenye simu sehemu ambayo ukifungua unakutana na dhamira yako..liwekee kengele kwenye simu kila kengele ikilia itakukumbusha hata kama umesahau hii inasaidia sana" anasena Babauta ni kweli inasaidia
Bruce lee chumbani kwake alikua na ubao ambao aliandika malengo yake kuhusiana na filamu na mafunzo yake anasema kila alipokua akiamka anakutana na ule ubao wenye malengo aliyojiwekea na akiona hivo anaongeza bidii kwa alichokua anakifanya..
Tujifunze kupitia bruce lee alichokua anakifanya
7: JENGA MATARAJIO
"kila nikipanda kitandani nilikua najenga picha kichwani kwangu jinsi nikikamilisha lengo langu maisha yangu yatakuwaje nilikua nafurahi sana na nilkua napata nguvu ya kuendelea kupambana" maneno haya yamesemwa na LEO MWANDISHI WA BLOG MAREKANI
Kila unapoweka lengo lako tarajia faida usiweke wazo la hasara kichwani kwako.. Hasara ni matokeo tu kama ya mwanafunzi anaesoma anatarajia kufaulu huwa haweki wazo la kufeli hata siku moja.
Mwaka 2017 ni wangu ni wako tutimize malengo yetu, tukumbuke kila mara tulilopanga kutimiza ndani ya mwaka huu ili kuepuka kumaliza mwaka bila kutimiza lengo lolote
By Jay Speed