Njia ya kupata mtaji kwa urahisi

Hagaih said

New Member
Jul 24, 2022
2
4
Kutokana na changamoto ya kupata mtaji hii nawaletea njia ya kupata mtaji hii imekua Njia rahisi zaidi ya kupata mtaji kwa urahisi bila riba riba ni uaminifu wako tuu. Chakufanya ili upate mtaji

Tafta watu wazima 12 ambao wanakazi zao rasmi wasiwe watu wenye njaa wawe na kazi zao ambazo wanauhakika na kipato chao, wasiwe na mikopo kama vikoba au tegemezi kwa wake au waume zao au wapenzi wao.

Wauganishe watu hao pamoja hakikisha wawe karibu sana wasiwe mbalimbali mfano nje ya mkoa au wilayani kiufupi muwe karibu sana mnaoweza kutembeleana kirahisi ili kurinda mtaji na pesa zetu kwa wavamizi .

Jiwekeeni kiwango maalum cha kuwekeza kila mwezi au wiki mbili hakikisheni hakuna mtu anayeshika pesa za mwenzake mfano kila mtu awe na kadi yake ya benki mtaanza kuchangishana kila mwezi au wiki mbili mtu anaweza kuchukua pesa yake kila baada ya mwezi au wiki mbili iwe na limit kwa muda na uwepo mfumo wa adhabu kwa mtu akichelewesha kumchangia mwenzake hii itakua njia bora zaidi na nyepesi kujipatia mtaji kwa urahisi zaidi na haitakua na masharti magumu wala riba yeyote.

Wepesi huu wa mkopo unapatikana kiurahisi zaidi but unataka mashrti. Madogo zaidi kama yafuatayo
1: Ifanye jamii ikuamini kwanza
2: Uwe na uangalau na kianzio cha laki au laki mbili hivi nikama mtaji kwa sababu inaweza kutumika kama emergency kipindi ambacho utakua huna pesa kumchangia mwenzako
3: Uwe na kazi ambayo inakuingizia kipato
4: Hii pesa sio ya kujaribia biashara utalia uwe na kazi ambayo unauhakika nayo asilimia 100%
5. Pesa hii sio ya kukopesha wala kutatulia matatizo ya ndugu na jamaa mfano mjomba kumeza wembewe mwache ameze usitoe iyo pesa

𝙈𝘼𝙏𝙐𝙈𝙄𝙕𝙄 𝙔𝘼 𝙈𝙏𝘼𝙅𝙄.
mtaji unahitaji kila mtu kupokea shilingi 1200000 sasa jobless kama mpo wawili mnaweza kuchanga ili msaidiane kurudisha pesa ya watu mtakua mnachanga kila mwezi 50000 ili kukamilisha 100000 ya kumchangia mwingine mwezi ujao au kama unaubavu wa kupata 100000 kila mwezi unaweza kupambana pekeako ili uchukue 1200000 pekeako chakufanya sasa kabla hujapata iyo laki6 au 1200000 hakikisha umetafta kitu chakufanya ambacho unakipenda na unahisi kitakupa faida.

mfano kama ni biashara ya nguo viatu au mgahawa au matunda vyoyote vile ili iwe rahisi kujiongezea mtaji wako haraka utafte mishe ambayo kila siku inaweza kukuingizia kuanzia 3500 elfu tatu miatano tuuh kwa mtaji wa 1200000 au 1750 kwa atakae chukua mtaji wa laki6
.

Biashara ambazo naweza kukushauri ufanye
A: Nguo
B: Viatu
C: Mgahawa/kuku
D: Matunda


Katika hatua hizi kama mdada wacha kula miguu ya kuku au kijana wa kiume acha maisha ya kuiga kushinda online bila kazi maalumu uwepo mitandaoni kuuza bidhaa sio kuangalia maisha ya mastaa
1: Acha maisha ya starehe huku pesa huna.
2: Punguza marafiki wasio na kazi maalumu
3: Penda kusoma au kujifunza kazi nje ya biashara zako
4: Siku isipite bila kubuni njia ya kuboresha kazi yako.

Mwisho niwatakie utekelezaji mwema
Hagaih said
 
Back
Top Bottom