Njia waliyoitumia wakenya kudai katiba mpya inaweza kuja kutumika Tanzania

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Binafsi kupitia wakenya nilijifunza kabisa kwamba katiba si kitu cha mchezo, katiba ndiyo maisha ya Wananchi vizazi na vizazi na katiba ndiyo Roho ya taifa lolote lile.

Wananchi waligomea katiba za watawala,waligomea kabisa kuundiwa sheria na watawala bila wao kushirikishwa!

Japo iligharimu maisha ya baadhi ya watu lakini mwishowe walikaa meza moja na kuunda katiba bora yenye maridhiano ya kila upande na ndio maana kwa katiba ya Kenya ya Leo kila mtu anaweza kua Rais na sio upande flani tu.

Watawala walijaribu kutumia nguvu kubwa sana kwa kutumia vyombo vya dola lakini wakenya walisema "hapana tunataka kabiba mpya na bora". Hakuna mwanachi aliyetishika wala aliyekubali kuonewa mpaka mwafaka ulipopatikana.

Hapa kwetu kitendo kile cha kupuuza maoni ya Wananchi na watawala kuwachagulia katiba nafananisha na Kenya na sijajua itakuaje Wananchi siku wakisema " NO tunataka katiba mpya na bora"
 
Back
Top Bottom