Njia rahisi ya kupunguza nguvu ya upinzani nchini.

ong'wafaza

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
243
100
Kwa maoni yangu upinzani wa kisiasa nchini unashamirishwa na mambo makubwa mawili:
1.Katiba ya nchi kuwa mbovu.
2.Mfumo mbovu wa utawala.
Mimi naamini kuwa wengi wanakuwa wapinzani kwa kuwa ama Mfumo wa utawala uliopo umewatema ili ufanikishe mambo yanayowapendeza watawala bila kujali madhara yanayowapata walio wengi ambao wako nje ya mfumo wa utawala,ama Katiba iliyopo haiwapi haki walio wengi.
Ukichunguza sana utagundua kuwa wengi waliofanya kazi zao kwa uadilifu mkubwa kwenye Chama na/au Selikari walitengenezewa zengwe na kufukuzwa na wengine kugeukia upinzani.
Kwa hiyo,kama katiba ya Warioba itapitishwa na mfumo wa utawala utafumuliwa,upinzani wa kisiasa utapungua sana.
Haya mawili yakifanyika naamini yatasaidia sana kudumisha pia amani miongoni mwetu badala ya njia zinazotumika sasa za kutumbua majipu,kuzuia mikutano ,kutunga sheria nyingi n.k.
Nawasilisha kwa mjadala mpana zaidi.
 
Back
Top Bottom