Njia rahisi ya kuhuisha [renew] leseni ya udereva

Njia rahisi ya kuhuisha [renew] leseni ya udereva

DENAMWE

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2019
Posts
878
Reaction score
906
Leseni yangu ya udereva imekwisha muda wake.

Je, naweza kuihuisha bila kwenda ofisi za TRA?

Namaanisha kuwa; je naweza kuihuisha kidijitali?

Mambo yapi yanahitajika?

========

OKTOBA 2025:

UTARATIBU WA KUHUISHA (RENEW) LESENI YA UDEREVA

Ukitaka kurenew leseni yako ya udereva fuata hatua zifuatazo:

Kwanza, ni lazima uwe na Akaunti katika mfumo wa TRA wa WALIPA KODI yaani TRA YAXPAYERS PORTAL. Na ili uwe na akaunti huko ni lazima uwe na TIN. Utatumia TIN yako kutengeneza akaunti ambapo utaweka Password. Utatimia TIN kama user name yako na password uliyoitengeneza kuingia kwenye mfumo.

Pili, Ingia kwenye Mfumo wa TAXPAYERS PORTAL kisha baada ya hapo Chagua sehemu iliyoandikwa MOTOR VEHICLE AND DRIVING LICENSES.

Tatu, tafuta palipoandikwa Application type. Ukipaona Click palipoandikwa RENEW

Nne, Ingiza taarifa zako Yaani namba ya leseni, Mkoa utakapochukulia na Mahali utakapochukulia, kisha click SEND.

Tano, Click print payment notice ili kupata control number ya kulipia. Mfumo utakuelekea uende TRAFFIC kwa ajili ya kupasishwa au kutestiwa. Baada ya kutoka huko ndio utaweza kuprint ile bill ya 70,000 kwa ajili ya KURENEW.

Sita, nenda kalipie bill yako kisha subiri kuptintiwa leseni yako.

Na usubirie siku ya kwenda kuchukua.

Ni matumaini yetu makala haya yatakusaidia kuongeza ufahamu juu ya mchakato huu

Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote
 
Ata mimi ime expire. Njia nyepesi ni kwenda TRA ni cheap. Kutumia vishoka gharama sana.
 
Na ukienda TRA, jitahidi udamke sa2 uwepo pale, ukienda sa4 vishoka wameshajaa.

Utapata control number, utalipia na siku ukipata msg ya kwenda kuchukua jitahidi uende mapema pia.

Unaweza hitajika kwenda Traffic,

Me nilienda ila sijui walichofanya, nilivofika nikampa karatasi la TRA aka update kwa system nikarudi TRA kuchukua control number.

Na TRA za leseni siyo zote, fuatilia mahali ulipo ni TRA ofisi zipi zinahusika na leseni za udereva.
 
Back
Top Bottom