Njia rahisi kabisa ya kuroot smartphone yako ya Android

Njia rahisi kabisa ya kuroot smartphone yako ya Android

gimp

Member
Joined
Feb 4, 2015
Posts
65
Reaction score
14
Hii ni app rahisi sana kutumia katika kuroot smartphone yako ya Android.

=====================================

Kipindi cha nyuma nilishawahi kuelezea katika blogu hii maana ya rooting. Katika operating system ya Android, rooting ni mchakato wa kufungua mfumo(system) wa Android ili kuweza kupata uwezo zaidi wa kuitawala smartphone yako. Operating system huwa na makabrasha(files and folders) ambayo huwezi pata uwezo wa kuyafanya chochote mpaka utapofanya mchakato wa rooting.

Unaporoot smartphone ya Android tunasema kwamba umepata "system privileges" ikimaanisha kwamba una vipaumbele vya kuweza kuitawala operating system ya simu yako. Hii itakuwezesha kufuta apps zilizopo katika system, kuzifanya apps unazodownload katika playstore kuwa apps za system(changing application softwares into system softwares), kubadili maandishi(fonts), kuweka operating systems zisizo rasmi(custom roms) na mengineyo mengi.

Kuna njia ambazo hutumika ili kuwezesha rooting kukamilika. Unaweza tumia programu za kompyuta au programu(apps) za Android, inategemea na njia unayochagua kutumia. Kuna baadhi ya njia ambazo hupunguza ugumu wa mchakato huu. Nitaelezea njia moja ambayo kwa sasa ni rahisi sana na inakubali katika smartphone za aina nyingi mno kuanzia Huawei mpaka HTC.

Njia hii hutumia programu(app) ambayo utaidownload na kuinstall katika smartphone yako, app inafahamika kama Towelroot. Kwa kutumia app hii, rooting ni mchakato wa dakika moja tu!. Nitaeleza hatua za mchakato huu.

1. Katika smartphone yako ya Android ingia katika internet browser uliyonayo na kisha tembelea address hii: http://towelroot.com au unaweza ingia moja kwa moja kupitia hapa. Kisha bonyeza alama ya lambda ili kuweza kudownload file la Towelroot.
Bonyeza lambda ili kuweza download towelroot.apk
2. Baada ya kukamilisha kudownload towelroot.apk, ingia katika settings za smartphone yako na kisha nenda katika security. Ndani ya security tafuta mahala palipoandikwa "unknown sources", hakikisha sehemu hii ipo activated.
Hutaweza install "towelroot.apk" kama unknown sources ipo deactivated.

3. Baada ya kukamilisha hatua ya pili, rudi katika internet browser yako kisha install "towelroot.apk".

4. Baada ya kufanya installation, fungua app ya towelroot katika menu yako. Baada ya kufunguka, bonyeza palipoandikwa "make it ra1n" .

Hakikisha simu yako ina mtandao(internet) wakati unafanya hatua hii.

5. Kama rooting imekubali katika smartphone, utatokea ujumbe unaoonekana hapo chini katika screenshot. Kama smartphone yako itakataa kuwa rooted kwa hii app itajizima na kujiwasha, hakutakuwa na madhara yoyote.
Kufikia hatua hii, smartphone yako inakuwa rooted.

6. Baada ya hapo, utahitaji kudownload app kwa ajili ya kupata ruhusa za kuingia katika system ya Android. App hii inaitwa Super User(SuperSU). Utaipata Playstore, ingia Playstore na kisha tafuta "SuperSU" halafu install.

7. Baada ya installation, fungua SuperSU na kisha update kwa kuchagua continue, updte kwa kutumia "normal".

8. Baada ya ujumbe unaoonekana hapo chini kukamilika kwa kusema "installation complete". Hapo utakuwa tayari umesharoot smartphone yako ya Android, tayari kuitumia kama Super User. Utahitajika kureboot na baada ya hapo unakuwa umekamilisha mchakato mzima

Ili kuangalia kama mchakato wa kuroot umefanikiwa kabisa, unaweza kutumia app ambayo inafanya kazi ya kuangalia root access kwenye simu yako, chagua langu huwa ni hii hapa ambayo inapatikana PlayStore "Root Checker". Lakini zipo nyingi sana playstore, chaguo ni lako.

Chanzo: Blogs
 
hii kingroot nayo taratibu zake za kuroot ni zipi
 
Kuroot simu yategemea na chipset ya simu yako...kwa mfano kuroot simu ambazo zinarumia SoC (system on chip) ya Snapdragon unaeza tumia app moja...same case goes to Exynos en Mediatek phones
 
Nina huawei y530,ilikuwa locked kwa tigo(ila nisha i unlock),vp kingroot itaweza kuiroot?
 
Si smartphone zote zinazokubali kuwa rooted kwa kutumia app hii. Lakini inasupport model nyingi sana za smartphones.
 
Ku-root cm, ku-root cm ndo nn hii kitu naickia sn ati? Na nn faida zake? (Msaada tutani)
 
Huawei y 300 imegoma.. pia y 530 imegoma nitumie app ipi waungwana
 
Nimejaribu kwa tecno F5 nikaambiwa this device isn't currently surpoted
 
mtakuja kuharibu cmu zenu hzo kuroot hakuna faida yoyote kama apps muhmu unazpata inatosha huko kungne mtakuja kulia tu...kama kuna vtu muhmu sana ambavyo huwez fanya kwa cmu mpaka uroot sawa zaid ya hapo utaharibu cmu yak
 
kabla ya kuroot fikilia hv...UNATAKA KUROOT KWA SABAB ZIP...KTU GAN UMEKOSA MPAKA UROOT....kama umekosa majbu....UCTAKE KUHARIBU CMU BURE BILA SABAB ZA MCNG KUNA MTU MPAKA LEO ANALIA CMU ISHAKUWA JANGA KUROOT HUKOHUKO HVO VTU NI ILLEGAL....
 
Back
Top Bottom