Njia rahisi 8 za kupata ajira popote ukiwa umemaliza chuo hizi hapa

Jun 8, 2016
83
651
Kutoka mwaka 2012 hadi 2015, kipindi cha miaka 3.. Nimeajiriwa na kampuni 7, full time, mshahara mzuri tu. Cha kushangaza hamna kampuni hata moja ambayo imewahi kusisitiza nioneshe cheti, baadhi huwa wanaulizia ila nikiiingia kwenye interview hua napita hadi wanasahau kuhusu cheti. Baada ya kuacha kazi yangu ya mwisho (sijawahi kufukuzwa, naacha mwenyewe) nime pata offer ya kazi zaidi ya sehemu 12, from August 2015 hadi June 2016 kipindi nnapoandika post hii, kwa sahivi nina kampuni 2 ambazo bado changa ila kwa pamoja zinaniingizia pesa kwa mwezi mara 5 kuliko kazi yoyote nliyowahi kufanya.

So kwanini naandika hii post? Watu nliomaliza nao form 4, mwaka 2009. Ndio wamemaliza chuo wengi wao mwaka jana(2015). Wengi either hawana kazi na wanatafuta au wamekwama kwenye kazi inaowalipa mshahara mdogo sana. Waliofanikiwa kupata kazi ni wale ambao wazazi wao wana connections, ambao baada tu ya kumaliza wameweka kwenye kitengo ambacho hawapendi ila inabidi tu wawepo. Na marafiki wengine kibao wanalalamika kua kupata ajira ni vigumu.. kupata ajira ni vigumu... so kwa kifupi tu ntaandika point chache, ambazo mtu yeyote akizifanyia kazi utapata employment almost any company you apply for, utakua na offer za kazi nyingi unachagua tu, na kila mwaka ukipenda utakua mshahara wako unapanda tu.

Toka nimeacha kazi nimepata offer za kazi kampuni kubwa kama clouds tv, star times, aggrey & clifford, na kampuni zingine ambazo siwezi kuzitaja maana walio ni offer wananifahamu vizuri. Na nikiwa na mda ntaandika zaidi kuhusu historia ya kazi zangu na kwanini niliacha kazi kote huko, actually kuna this one place i was employed (sija include kwenye hizo kampuni 7 nilizofanyia kazi) hii kampuni niliacha kazi baada ya siku 3, mwajiri akaniita mara tatu ofisini kwake kuniomba nibaki na ku offer kuniongezea mshahara mara 3 (kutoka laki 3, ikaongezeka hadi laki 5 na 50) lakini bado nikaacha hiyo kazi after 3 days (kumbuka hapa sina cheti hata kimoja, hata cha form 4 nilikua sijachukua kwa kua sikumalizia ada).

Ukweli kuhusu cheti ni kwamba kuna sehemu na sehemu kinahitajika kama kuwa daktari, ama mwanasheria ila most of the jobs watu wanazotafuta na hawapati, vitu vinavyohitajika ni uwezo wako tu wa kufanya kazi, ntakuelezea jinsi ya kuonesha huo uwezo.

Anyway enough chitchat... Below ni njia ambazo ukitumia utapata kazi unayotaka almost anywhere.

1) How to battle the experience factor (Jinsi ya kupambana na wanaotaka uwe na experience kabla ya kazi)

This is the easy one, hapa pa rahisi kinoma.. itakuchukua mda kama miezi sita or less (inategemea na ufanyaji kazi wako) lakini kupata experience kabla ya kuanza kazi ni muhimu, siri ya hapa' experience sio lazima uwe umeajiriwa before, wengi wanasema hivi, ila ukifuata hii njia ntayokutajia utapita na experience yako utayoipata. Ukimaliza chuo tu achana na watao ungua jua kutafuta kazi, tafuta experience kwanza.

-Jitolee bure kabisa popote, usiombe ulipwe. hamna ataekataa wewe kujitolea, for example unafanya accounts, tafuta ndugu yeyote mwenye kampuni yoyote "iliyosajiliwa"

Jitolee bure, mueleze unatafuta experience so utafanya kazi bure yoyote siyo lazima iwe hata ya accounts we mwambie utafanya yoyote. Kama huna ndugu jipangie ratiba kuingia ofisi yoyote (chagua tatu kwa siku) na waambie the same. Ukiwa smart siku ya kwanza tu unapata (If needed ntaandika how to aproach any situation bila kukataliwa... someday).

-So umeomba umepata, usikwame hapa fanya hii kazi maximum miezi miwili kwa nguvu zako zote. kama mda wa ofisi saa mbili, wewe saa moja upo pale, kama mda wa kutoka saa kumi na moja wewe upo hadi saa moja usiku. ila baada ya mwezi mmoja au miwili acha, wape sababu yoyote iwe nzuri lakini (nahama mkoani, narudi shule, ila usidanganye sana), what is important ni kuondoka in good faith na uwe na contacts za mmoja au wawili wa hiyo kampuni (ntaelezea kwanini baadae). Najua wengi watataka kukupa kazi wakiona ufanyaji wako wa kazi, ukitaka chukua ila ndo itakua mwisho wako huo, siku unaachishwa for any reason huna sehemu ya kwenda. i sudgest acha hiyo, move on to the next one. So Rudia hii process mara 3 hadi 6 for better results...

-Siri ya hapa ni kuonekana kama umefanya mda mrefu, usianze mwanzo wa mwezi, nenda mwezi wa nne tarehe 15 hadi mwezi wa tano tarehe 15, hapa itaku aumefanya miezi miwili. au nenda mwezi wa nne tarehe 25 hadi mwezi wa sita tarehe 2, hapa umefanya miezi mitatu (kwenye CV, under experience unaandika intern from June -August). Kuna njia nyingi unaweza uka stretch kazi ya siku 90 kuwa una experience zaidi ya mwaka mmoja ambazo nikipata mda ntaelezea.

{side note: usiombe hela yoyote ukiwa kwenye kipindi hiki, sijui utapataje hela ila figure it out, but most of the time kama percent 80 hivi ya sehemu utapoomba kujitolea utapewa hela za kula na nauli baada ya wiki tu ya kuona ufanyaji wako wa kazi}

Ukimaliza kujitolea kampuni zako 3 –6.. Hii ni experience tosha, huhitaji yoyote nyingine. With this alone ukienda enterview 5 utapata kazi sehemu moja wapo guaranteed. Important sasa ni kuweka your contact kwenye kila kazi ulipofanya (namba za wahusika kila kampuni) na lazima uwe umeacha kwa good terms incase wakipiga utasifiwa sana, hawajawahi kupiga in my case ila mtu mmoja nilimpa hii njia wakapiga simu.

Also hizi kampuni utaziandika under experience kwenye CV yako, kwenye format ifuatayo

(n.b these are samples)

2) Kampuni inapenda "the multitasker" (mtu anaeweza kufanya vyote)

Again this is very easy hata sijui kwanini watu hawa apply. Kwenye CV yako always have a section ya "other skills" or kitu kingine kama hiki kinachoweza onyesha skills zako zingine. Kwa mimi other skills nikikuonyesha CV yangu imejaa page nzima moja... Ukiulizwa kwanini, wewe sema unapenda sana kujifunza, na kuwa haulali siku bila kujifunza kitu kipya (hii inabidi iwe kweli kwa ushauri wangu, jifunze kitu kipya kila siku, but for the purpose of this post achana na hilo).

Unapataje other skills? Well tupo kwenye ulimwengu ambao ni rahisi sana kujifunza chochote. Best source nnayotumi ni youtube. YouTube ni mtandao wa video wenye kila kitu utachoweza kufikiria wewe... as long as its legal kipo humu ndani, wewe jifunze chochote then andika kwenye other skills. Vitu kama photo editing kwenye photoshop' unaweza ukajifunza ndani ya siku mbili, basic za ku edit picha kwenye photoshop, alafu kwenye CV andika "Basic skills in photoshop editing". Ndo rahisi kihivyo, believe me kama hau apply kwa ajili ya graphics hutotumia hiyo photoshop skill, 98% ya other skills huto kuja kuzitumia hata mara moja.

Mfumo wa kuandika kipengele cha other skills ni as follows

3) Cha kufanya kabla ya interview (Muhimu)

Hapa sasa umetuma CV yako na umeitwa kwenye interview, kwa mimi sijawahi kwenda kwenye interview na nikakosa kazi niliyoitwa, kuna mda nikawa nafanya kama test tu niende alafu nione kama ntapata, alafu napata. kuna mtu nlimpa hizi njia akatumia sehemu tatu, sehemu mbili akaitwa aanze, akaishia kuchagua tu wapi atalipwa zaidi.

I) Fanya Research ya hiyo kampuni unayo apply.. Chukua siku nzima kufanya research ya hiyo kampuni siku moja kabla ya kwenda kwenye enterview, ujue ni nini inahitaji, kwanini wanataka ajiri, nini kimekosekana. Kampuni inaajiri ili either kuziba pengo au wanaona kuna upungufu flani kwenye kitengo husika. So hawatoi ajira ili kukusaidia wewe upate kipato, THIS IS VERY IMPORTANT . Narudia, kampuni hai ajiri ili kukusaidia wewe upate kipato au usolve matatizo yako, ina kuajiri ili ku solve matatizo yao.

So kamwe usiende kwenye interview ili kujielezea wewe, DO NOT DO THIS. Kosa ndo hapa kubwa, hii ndo sababu kwanini haupati kazi kama una tafuta, mtu anaenda enterview ili kujielezea sijui "mimi ni mchapakazi, mimi naweza ABC...... achana na hayo....

Inabidi useme vitu kama "naona kuna ukosefu kwenye sector ya customer care kwa kipindi cha miezi sita, na kampuni ikitoa customer service nzuri ndo wateja wanaiamini, so mi naweza nikasaidia kampuni yako kwa kufanya ABC" This is the right way. This alone will get you the job kama ukiweza fanya research vizuri na kuona nini kimekosekana.

kuna siku kulikua na kazi ya social media marketing, nilitafuta hadi mtu ambae anafanya kazi kwenye kampuni husika na kumuuliza kampuni inahitaji nini, akaniambia "ni kweli wamesema wanatafuta mtu wa ku manage social media, ila ukweli wanahangaika sector nzima ya marketing"… long story short nilifanya kazi hapo kwa miezi minne kama marketing manager.

4) Fanya kazi unayo apply kabla ya kuajiriwa

Hii na prefer kufanya baada ya interview, kama wewe ni project manager (mfano) na ndio una apply for kazi ya u manager, tafuta njia ya kuonyesha uwezo wako kabla haujaanza kazi, kitu kama andaa report then mtumie boss. Au kama wewe ni marketing, ukitoka tu kwenye enterview nenda katafute mteja kwa ku market hiyo kampuni, au andaa marketing plan. Hii step ndio ngumu kwenye baadhi ya sector. Lakini hii ndio wazungu wanaiita "nail in the coffin".

Ukiweza fanya kazi kabla ya kuajiriwa muajiri kama amekwama kwenye kuchagua watu watano na wewe mmoja wao, lazima atakuchagua wewe kwa sababu ameona uwezo wako, wengine wote walipo hapo hajui uwezo wao, lazima atakupa hata mwezi mmoja wa trial. Mwezi mmoja unatosha kabisa kumfanya akupe mkataba wa mwaka au zaidi.

Ukiweza kwenda na kazi ambayo unataka kupewa, uwe umeshaifanya then interview ikiisha tu unamuonesha, unaweza ukapewa kazi hapohapo. Especially kama umefuata maelezo yaliyopita ya hapo juu. imenitokea more than once, kuna watu nje wanasubiri kufanyiwa enterview ila muajiri ananiuliza mimi naweza anza lini.

-------------------------------------------------------------------------------------

Okay... nmechoka kuandika.... this post imekua ndefu kuliko nilivyotegemea.. Na mda unaenda I have a lot to do. So naishia nusu kwa sasa.. Kwa ataehitaji niendelee tafadhali nijulishe kwa kuacha comment hapo chini, na kama una swali lolote pia uliza ntajitahidi kujibu. Kuna mambo mengi sana, kama ya kupata mshahara mwingi zaidi ya wanaotaka wakupe bila kuwaomba, na pia njia za kufanya kazi kampuni zaidi ya moja kwa wakati mmoja, promotions na mengine for next time.

Nimeshasaidia watu wachache kupata kazi, I hope hii itamfikia mtu husika na kumsaidia yeye pia kupata kazi yake anayo ihitaji. Sijawahi kutumia cheti hata mara moja kupata kazi na wala nikitafutwa kupewa kazi sijawahi ulizwa kuhusu cheti natafutwa kisa I am the most qualified person ya hiyo sector wanaemjua (ukweli ni kwamba kuna wengi zaidi who are more qualified) ukitumia hizi njia vizuri utapata kazi yoyote unayoitaka mostly kwenye private sector, ila I was offered kazi hadi serikalini for 900,000 (laki tisa) + gari la kutembelea na sehemu ya kuishi, nikakataa. This too ni maongezi ya siku nyingine.

Kwa ataekua ana wonder mi nipo kwenye sector ya I.T, ila nmesaidia watu wa accounts, project management, H.R, presenter pamoja na marketing executive kupata kazi in a very short time, ukitumia hizi njia vizuri hautokosa ajira, this is a fact.

(Hii post itakua updated nikikumbuka mambo muhimu ya kuongeza)

MUENDELEZO: BOFYA HAPA
 
IT ni uwanja mpana sanaaa, kuna haja ya kubobea katika nyanja moja effectively??
Inategemea what is your end goal!.. Ni muhimu sana kuwa na end goal in mind, kama end goal yako ni kuajiriwa kwenye nyanja yako na mshahara mzuri for the rest of your life then unahitaji kubobea kwenye hiyo nyanja... Lakini kwa wakina mimi wenye nia ya kujiajiri mwisho wa siku, haina haja ya kubobea popote...
 
Aisee hii post imenirudishia imani ya kupata kazi soon...kaka kuna semina ya Daraja la mafanikio 18th June 2016 JNICC nadhani unaweza kuwa mzungumzaji na mhamasishaji mzuri, tafadhali kama hutojali wasiliana na AMCHAM TANZANIA.
Samahani unaweza eleza vitu kama kiingilio, itaanza sangapi na kumalizika saa ngapi, wahuska ni watu gani,
 
Gud kaka nmekuelewa sana, akina sisi tunasukumwa kutafuta kazi kutokana na stress na ugumu wa maisha ndio maana hata tukiingia kwenye interview tunajielezea sifa zetu badala ya kuelezea tutafanyia nini kampuni ama taasisi, pia uvivu wa kufikiri ndio inatupelekea kutegemea mishahara kuliko kujiajiri, asante na ubarikiwe kwa kutufungua.
 
Aisee hii post imenirudishia imani ya kupata kazi soon...kaka kuna semina ya Daraja la mafanikio 18th June 2016 JNICC nadhani unaweza kuwa mzungumzaji na mhamasishaji mzuri, tafadhali kama hutojali wasiliana na AMCHAM TANZANIA.
Huyo ni miongoni mwa waandaji wa hiyo semina, ina maana hamfamiani?
 
Mimi ni mhudhuriaji tu, hatufahamiani.
Hata miye huwa nahudhuria, ila mambo anayoongea yanaweza kukusaidia, lakini ni vizuri kuchuja na kuwa makini. Kwa mfano anaposema alipata kazi serikalini yenye mshahara wa laki tisa + gari ya kutembelea na mahali pa kushi - kuna upungufu ufuatao: Mshahara wa Serikali hauwezi kuwa fixed kiasi hicho yaani 900,000/= bila sent; gari unayopewa sio ya kutembelea bali ya kazi na most of the time inaendeshwa na dereva ambaye ni mtumishi, yeye ndo anakuwa na gari muda wote na ukifika kazini asubuhi gari hiyo inakuwa chini ya TO; siku hizi Serikali haina nyumba za kuwapa watu tena mtu mwenyewe mwajiriwa mpya, hata kuthibitishwa kazi bado !!! Aidha, ngazi hiyo ya mshahara ni Afisa daraja la II, ambaye bado ni mgeni katika utumishi, hawezi aminiwa kiasi hicho labda kama ni Kampuni Bimafsi.
 
Hata miye huwa nahudhuria, ila mambo anayoongea yanaweza kukusaidia, lakini ni vizuri kuchuja na kuwa makini. Kwa mfano anaposema alipata kazi serikalini yenye mshahara wa laki tisa + gari ya kutembelea na mahali pa kushi - kuna upungufu ufuatao: Mshahara wa Serikali hauwezi kuwa fixed kiasi hicho yaani 900,000/= bila sent; gari unayopewa sio ya kutembelea bali ya kazi na most of the time inaendeshwa na dereva ambaye ni mtumishi, yeye ndo anakuwa na gari muda wote na ukifika kazini asubuhi gari hiyo inakuwa chini ya TO; siku hizi Serikali haina nyumba za kuwapa watu tena mtu mwenyewe mwajiriwa mpya, hata kuthibitishwa kazi bado !!! Aidha, ngazi hiyo ya mshahara ni Afisa daraja la II, ambaye bado ni mgeni katika utumishi, hawezi aminiwa kiasi hicho labda kama ni Kampuni Bimafsi.

Hata mimi pamoja na kupenda seminar ya mtoa mada hapo nilitia mashaka labda kama alimaanisha Taasisi /Shirika la Umma mfano NHC, EWURA, n.k
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom