Njia pekee ya kuisaidia jamuhuri ya muungano wa tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njia pekee ya kuisaidia jamuhuri ya muungano wa tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JOMAM, Aug 24, 2012.

 1. JOMAM

  JOMAM JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kwa mda sasa tumekuwa katika mazungumzo ya jinsi ya kuliweka taifa letu,na namna bora ya kuendesha mambo
  kimsingi binafsi yangu ninafikiria mambo kadhaa ambayo kama tukiyafanya kuwa msingi wa taifa letu hata katiba tutakayo itengeneza basi itakuwa na maana kwetu kama ifatavyo
  1. sera ya taifa;taifa lazima liwe na sera ambazo ndizo zitakazotumika kama muongozo wa utekelezaji wa mambo katika nchi,sera hizi zinakuwa miongozo ya viongozi wakiwa madarakani na wananchi katika namna bora ya kuchangia huduma ya maendeleo,hivyo ilani za vyama vya siasa zitumike si kama sera za taifa bali namna bora ya kutekeleza sera zile zilizopitishwa na nchi. Hii inatupa pia nafasi ya kutofata hisia za mtu binafsi na taifa kukosa mwelekeo;mathalani anaingia kiongozi anasema safari hii nimefuta mtihani wa kidato cha nne akija mwenzake anasema nimerudisha,safari hii nimefuta michezo mashuleni akija mwingine nimerudisha,huku ni kulifanya taifa kuwa bendera fata upepo.
  2. maadili ya taifa; yako wako wapi maadili ya taifa yanayotuongoza kama taifa sisi kama viongozi nasisi kama raia tusio viongozi,maadili ambayo kama tukifanya kinyume na ikathibitika basi tunakua na lakujibu,pale ambapo viongozi wetu wanaahidi kitu ambacho hawawezi kukitimiza wanakuwa na la kujibu mbele ya jamuhuri,maadili haya yatubane hata namna ya maisha tunayoishi hasa viongozi.
  3. Kutoruhusiwa kwa viongozi wa serikali kuwa viongozi wa vyama vya siasailikutoa nafasi kwa chama kuwawajibisha viongozi wake wanapokosa hususani raisi wa nchi,kwakuwa raisi ni mjumbe wa kamati kuu ya chama cha siasa basi anaouwezo wa kueleza au kujibu ya serikali ndani ya chama lakini iwapo atakuwa mkuu wa chama kilichomweka madarakani basi hana wa kumuuliza sana kwani pande zote anakua anaogopwa,ndo hayo yanayoweza kumpa mtu jehuri ya kumweka apendaye na kumwondoa atakavyo,mathalani ikiwa rahisi atakosana na spika wa chama chake kwa sababu za kitendaji hanauwezo wa kumwondoa kiongozi huyo mkubwa lakini atatumia chama yeye kama mkuu wa chama. kutenganisha mamlaka hizi zilizo ndani ya nyumba moja kutasaidia viongozi kutokuwekana au kuwabeza maskini
  4. kuwepo kwa usahili wa hadharani kwa watu wanaopitishwa katika mchujo au kuteuliwa serikalini iwe inafanywa na kamati maalumu ambayo haiusiani na siasa,bodi ya wataalamu itakayosema hawa wanafaa kuteuliwa baada ya usahili mkali wa hadharani unaowafanya wananchi waone kupitia vyombo vya habari,hapa tutaondoa masikitiko ya watu na kuwekana kwa viongozi,hii ifanyike hata pale pakugombea bodi ikate majina kwa competence zao kisha iacha majina ya wachache watakao chujwa na chama husika kwa vigezo vya kichama kisha kuruhusu wajumbe kumpata wamtakae
   
Loading...