Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,777
- 6,907
Wanasema 'politics is the art of compromise'. CCM wanalitambua hili kwa kina kwa maana wameshuhudia na kuwa part ya negotiations nyingi tu za kisiasa kuanzia huko Burundi, Rwanda, Angola, Kenya, Zambia, nk. lakini mfano mzuri kuliko wote ni Afrika Kusini.
Kuna uzi bora kabisa unaoelezea hii dilemma kubwa inayoikabili CCM. Ni hali ya sintofahamu ya nini kitatokea tukipoteza madaraka ya kuongoza nchi hii. Zamani tulikuwa tunaaminishwa kuwa kuwapa wapinzani ni kuiuza nchi na kuiingiza kwenye machafuko na najua ni propaganda inayoendelea kutumika ila ukweli ni kuwa kinachoisumbua CCM ni WOGA wa kufutika na kupotea pale itakapopoteza mamlaka ya kuiongoza Tanzania. Hii naiongelea katika top level ya CCM na wale wastaafu, hawa wa chini hawana maslahi mapana katika mfumo wa sasa.
Nisingependa kurudia alichokisema Pascal Mayalla lakini unaweza kukisoma hapa CCM kutumia Hooks & Crooks Kushinda Chaguzi, Inajua Ikishindwa Ndio Itakufa Jumla, Itakubali?. Ni uzi bora kabisa ambao nashangaa una page 3 tu wakati ndiyo center ya kila kinachoendelea Tanzania toka mfumo wa vyama vingi ulipoanza.
Upungufu wa uzi wa Mayalla ni kuwa hakutoa suluhisho na hilo ndiyo naenda kufanya. Kama ilivyotokea sehemu nyingine duniani, tunahitaji msuluhishi ambaye pande zote wanamuheshimu. Kwa usalama wao na mustakabali wa taifa hili, wapinzani inabidi wachukue initiative ya kuwatafuta na kuwashawishi hao watu na hizo taasisi ambazo wanajua CCM wanaweza kuwasikiliza. Hii issue wala haihitaji kufanyika waziwazi kwa sababu CCM wataipiga vita kama ambavyo walipinga uchunguzi wa nje kwenye shambulio wa Tundu Lissu. Hawataki kuonekana kuwa wameshindwa kuiongoza nchi which is understandable kwa sababu nalo lina athari zake.
Ninachoamini na ni kitu nimekitafakari kwa muda mrefu ni kuwa viongozi wengi wa juu wa CCM wako tayari kutua huu mzigo wa chama waende kufanya mambo mengine ila wanahitaji kuhakikishiwa siyo tu usalama wao lakini pia wa mali zao. Hilo likifanyika, mtaanza kuona kamba inaanza kulegezwa taratibu. Otherwise, hakuna anayetaka chama kimfie mikononi mwake kwa sababu repercussion (athari) zake hazikubaliki!
Nayasema haya nikiamini nina kipaji cha maono kwenye mambo ya siasa. Sijisifu, ni fact! Hiki ndicho nilisema March 22, 2007 (YES, 11 years ago!) kwenye uzi huu wa kuhusu Mugabe Zimbabwe: The turmoil, reconciliation, and the future!
"Mkira, I doubt Mugabe na supporters wake ikiwemo tz, namibia, SA, angola, DRC etc watakubali kuona Mugabe anaondoka through mass protest au njia yoyote yenye nature hiyo kwa sababu itapeleka message kwenye nchi zote hizi kwamba 'kama hatuitaki hii serikali yetu tunaweza kwenda kuprotest hadi waondoke' na sidhani kama wako tayari kuona hiyo message inatolewa. Ni kweli wengi wanaona Mugabe ni liability sasa hivi lakini watamanouver ili ang'atuke kwa heshima, lakini hatatoa sign yoyote ya kuback down, at least for now. Lakini best believe land reform itabaki (na mimi personally naisupport by any means necessary) na pia mapigo ya moyo ya Morgan Tsvangirai yatasimama (an ugly fact about politics)."
Swali ni nani atawahakikishia viongozi wa CCM ambao wameshafaidi matunda ya nchi hii kuwa yaliyopita si ndwele....?
Nawasilisha mada.