Njia nyembamba (Simulizi mpya by SteveMollel)

Steve wewe ndo mtunzi, unajua fika ni simulizi gani itatubamba mule mule! Ebu fanya kuliamusha dude lenye kusisimua mithiri ya Baradhuli mwenye mkono wa chuma.

Mimi na watu wangu wa nguvu Shunie Tumosa kisukari etc tupate kujilamba kwa mautamu!!
 
Habari zenu wapenzi wote mnaofuatilia simulizi hii ya NJIA NYEMBAMBA. Samahanini kwa kukawia kutuma simulizi yetu na yote ni kwakuwa nabanwa na ratiba.

Huwa nauza simulizi zangu huko mitandaoni, ila kwa hapa sitauza simulizi yangu hata moja. Kila nitakapokuwa napata muda nitakuwa natuma simulizi tuendeleze kupeana raha.


Sasa turudi kwenye mada takiwa, kwa mujibu wa ratiba yangu ya sasa ya utumaji wa simulizi kwenye mtandao (kwa wale matomaso wanaweza pitia page yangu ya instagram: simulizi_za_series), simulizi ya NJIA NYEMBAMBA imekaa kando kwakuwa imeshakwisha msimu wake wa pili ambao ndio huo nimekomea hapa Jamii Forums. Hivyo itarudi tena kwenye msimu wake wa tatu baada ya muda kidogo.


Hivyo basi, kwakuwa itachukua muda kurejea hapa msimu wa tatu, nilikuwa nina pendekezo ningependa lifikisha kwenu. Kwa wakati huu ambao tutakuwa tunangoja MSIMU WA TATU, naweza nikaleta simulizi zangu zingne kuvutia muda. Nazo ni kama zifuatazo mwaweza zichagua:

(a) ANGA LA WASHENZI

(b) MKUFU WA MALKIA WA GOSHEN

(c) JOANA ANAONA KITU USIKU.


Au nyie mwaonaje? unaweza ukachagua hapo ipi twende nayo. Nimeona ni bora zaidi kwakuwa hizo simulizi zimefikia mbali, pili ratiba zipo upande wake kwa kiasi kikubwa.


Karibuni.
Mkuu tuwekee Mkufu wa Malkia wa Ghoshen
 
Back
Top Bottom