Njelu Kasaka uko wapi? Kagombee jimbo la Lupa kupitia CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njelu Kasaka uko wapi? Kagombee jimbo la Lupa kupitia CHADEMA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by akelu kungisi, Apr 20, 2012.

 1. a

  akelu kungisi Senior Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni miaka takribani kumi na ushei hivi aliyekuwa mbunge machachari na baadaye akawa waziri wa kilimo, mara akawa mkuu wa mkoa Tabora amepotea katika uwanja wa siasa.
  Ukichunguza kilichomuondoa katika siasa za wakati ule ni kwamba alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali na alisimamia ukweli daima. Naam, demokrasia ilivizwa na chama tawala CCM, kwa hiyo yeyote aliyekuwa anakosoa chama kinapokosea alikuwa anawajibishwa!
  Hoja kubwa iliyomuondoa kwenye ulingo wa siasa na wenzake kama akina Jenerali Ulimwengu ni ile amabayo leo hii imeibuka upya hasa visiwani ya kutaka kuwa na seikali tatu. Yeye alikuwa kinara wa kundi la wabunge waliojulikana kama G55. Kwa busara za Baba wa Taifa Nyerere kundi hili lilizimwa na wengi waliokuwa vinara wakapewa madaraka lakini mwisho wao ukawa mbaya kisiasa, ni wachache tu mfano wa Sam Sitta ambo bado wadunda.
  Maranyingi nimeonana na huyu mzee na nimefanya mahojiano naye, nilichogundua ni kuwa ni mtu ambaye ana maono ya mbali yanayoonyesha mapinduzi ya kifikra na ukombozi wa nchi yetu Tanzania kiuchumi, kisiasa n.k. Mara chache huwa anatoa makala zake katika gazeti la RAIA MWEMA na maranyingine anatoa katika gazeti la RAI.
  Ukizisoma makala zile unaweza kumtafuta na kumwambie mzee wakati ni huu, chama chenye maono na itikadi ya ukombozi kwa Watanzania ni CHADEMA! Mawazo yako na ushauri wako waliokuwa wanaupinga na kuukataa sasa waweza kuutoa ukiwa katika mfumo huru wa kichama unaoongozwa na viongozi wenye fikra kama zako.
  Anza kujiandaa na mikakati ya kuwakomboa wakulima wa tumbaku kule Lupa Tingatinga. Mpiganaji wa ufisadi Mwambaraswa amevizwa na magamba, hatumsikii wala hatuioni michango yake bungeni zaidi ya majungu nafitina za ndani kwa ndani kwenye chama chao!
  Kokote uliko upatapo ujumbe huu hima usichelewe kutimiza haja na matakwa ya watanzania
   
 2. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sikuungi mkono kabisa katika hilo. Huyo unayemtaja alishataka kugombea huko kupitia CUF.. Halafu hilo kundi la G55 ni ***** mtupu wahauini wakubwa hao. Hebu nitajie na wengine waliokuwa hilo kundi.
   
 3. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mwache apumzike
  Wa kutumwa ni vijana na sio wazee
  OTIS
   
 4. a

  akelu kungisi Senior Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Revolutionary,
  Uhaini wao ni upi ni upi katika hoja ile? Hapa ujadili mantiki ya hoja, hata nikikutajia watu hao haitahusiana na kiu yangu ya kumtaka mzee huyu akalikomboe jimbo la Lupa.
  Kwamba alikuwa CUF, ni hoja aliyokosa mashiko! Alikuwa anatafuta uwanja au chama ambacho kingeweza kumpa uhuru wa kufanya siasa za kiukombozi kama za CHADEMA!
  So far, CHADEMA was not popular those years, ni imani yangu kuwa iwapo CDM kingekuwa na matawi Chunya kama sasa Njelu Kasaka angepita. Na uelewe kuwa angepita si kwa sababu ya umarufu wake bali ni kwa sababu ya chama na jinsi kinavyokubalika.
  This man deserves to contest in the coming election!
   
 5. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Njelu Kasaka ni choka mbaya. Hafai kugombea, labda awe mwanachama wa kawaida tu.
   
 6. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hatumtaki kwani hakuna mtu mwingine wa kugombea zaidi ya njelu?

  chadema kuna vijana wachapa kazi kibao huyo mzee hatuna haja nae

  tunataka wanamapinduzi wa kweli
   
 7. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  Amezeeka mno, haiwezi kasi ya sasa. Abaki CCM au CUF, au akienda CDM awe mpiga kura tu
   
 8. a

  akelu kungisi Senior Member

  #8
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kashaijabutege & Kiduku,
  Hoja ni kuangalia ni nini mtu anacho kwa bichwa ( akili ). Umri sio kigezo cha kum-disqualify mtu abadani!
  Kiduku, Watanzania hawataki pesa, kuchoka kifedha kwa huyu mzee kisiwe kigezo cha kumkataa!
  Hata hivyo CDM haiwezi kuwa na vijana tu, inashauriwa popote pale kuwa penye wakubwa haliharibiki jambo!
  Kwanza huyu mzee bado ana nguvu zake, na anaonyesha anaweza kupiga kazi! Hakuna kipengele chochote katika katiba ya CHADEMA kinachowabagua watu waumri kati kama Kasaka
   
 9. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #9
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  kama sijakosea huyu mtu alishatoka CUF na kurudi CCM muda mrefu, aende tena CDM? No pls mwache apumzike na hana mashiko kwa sasa
   
 10. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asante kwa mawazi yako mazuri, ila siungi mkono hata kidogo. Taja majina na upuuzi waliofanya hao G55 tuone, kama hujui hao ndio waliotaka kuvunja muungano.
  Labda kigezo cha kumchagua kingekua ni mazuri aliyoyafanya kwa kipindi chote alichokua mbunge jimboni lupa kwa miaka kadhaa kupitia CCM, hebu tutajie bwana mkubwa.

  Otherwise hatutaki kurudisha wastaafu kazini wakati kuna vijana wachapa kazi.
   
 11. M

  Molemo JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ana miaka 76 sasa!
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ni kikongwe nasikia hata meno yameanza kutoka
   
 13. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wewe Akelu Kungisi ndiye Mzee Njelu Kasaka mwenyewe. Hakuna mtu mwenye akili timamu toka wilaya ya Chunya anaweza kumpigia debe huyu punda mzee zaidi ya mwenyewe na wanae.
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kwa sasa tunaweza mtumia kama mshauri tuu not otherwise!
   
Loading...