Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,997
- 20,329
Katiba ya Tanzania na NJAA ya vijana kuhamia vichwani ni angamizo kwa taifa, kudumisha ujinga ni msingi wa utawala wa mafaa wa ccm chini ya hapa kazi tu huku kazi hakuna na njaa zipo vichwani badala ya tumboni.
Katiba ya Tanzania inatamka kwamba Mamlaka kuu ya nchi inatoka kwa Wananchi.Wananchi ndio huiweka au wanaiweka Serikali madarakani na kuikabidhi majukumu ya kuunda dola,
Sambamba na hilo kwa kutumia demokrasia ya uwakilishi, Wananchi haohao wanawachagua wawakilishi wao (Wabunge) ili waisimamie Serikali yao katika utekelezaji wa majukumu hayo.
Ili kufanikisha, bunge huishauri Serikali, huidhinisha mapato na matumizi nchi kuanzia senti moja hadi trilioni (bajeti) yake na hata kuihoji au kuikosoa na zaidi kuiondoa serikali hiyo madarakani. Hali kadharika bunge hutunga sheria zinazoongoza nchi na zinapaswa kuheshimiwa na mihimili yote ya dola na wenye dola mwenyewe (Wananchi).
Kimsingi kupitia bunge ni kama wananchi hutoa mwongozo wa nini serikali ifanye (Hadidu rejea)
Kwa bahati mbaya sana sivyo ilivyo hapa Tanzania kwa bunge la serikali ya awamu ya Tano. Serikali inalisimamia na kuliongoza bunge kutoka kusikojulikana. Aliyeajiriwa anampangia mwajiri yale atakayo yeye kuyafanya, halafu kwa kuwa mwajiri ni maamuma, anashangilia eti Mwajiriwa wake ni excellent.
Hapa ndipo naikumbuka Tamthiliya ya Adui wa Umma (An Enemy of the people) iliyoandikwa na Henry Ibsen huko Ulaya miaka ya 1700
Katika moja ya mijadala flani kwenye viunga vya wenye akili, jamaa yangu mmoja anasema, definition ya government of the people, for the people, by the people ilikufaga kifo cha kawaida zamani.
Katika Tamthilia hii kuna Mhusika Mkuu anaitwa Dr.Stockman, Baada ya kupitia masahibu Mengi akiitetea jamii yake aliishia kuitwa na hao anaowatetea kuwa yeye ni adui wa Umma.Katika mkutano wa hadhara ambao wakandamizaji wa jamii (Wananchi) waliwashawishi wanajamii wamwone mtetezi wao (Dr.Stockman) kuwa ni adui yao.
Mlevi mmoja akiwa amelewa bila haya, peke yake alisimama kumuunga mkono Dr.Stockman. Hapa Dr.akavumbua jambo jipya kwa Muda mfupi sana kuliko uvumbuzi uliomwingiza matatani aliofanyia utafiti kwa muda mrefu sana. He came with a new great discovery that "In any poor society like what he belonged, THE MAJORITY ARE FOOL"
Wananchi wamenyang'anywa haki ya kusikiliza,kutazama na hatimae kujua kama bunge lao linawasimamia vyema waajiriwa wao, lakini ajabu na kweli wapo wanaoshangilia. Wananchi wamenyimwa haki ya kutoa maoni ambayo inageuzwa na kuitwa uchochezi, ajabu na kweli wapo wanaoshangilia. Wananchi wamenyimwa haki yao ya kikatiba ya kukusanyika na kushiriki mijadala ya wazi ya kisiasa bila sababu za msingi, ajabu na kweli wapo wanaounga mkono na kushangilia kitendo hicho.
Nakuhakikishia ikitokea kwamamlaka ambayo katiba ya Jamhuri imempa Rais Magufuli, leo atoe ushauri (amri) kwamba Bunge liwe live, shughuli za kisiasa iwe ruksa, hawa vijana wenzetu wa ccm waliohamishia njaa kichwani utawaona wanarudi na kuimba nyimbo za sifa eti Rais wetu ni msikivu sana na mpenda demokrasia
Chochote unachokiweza katika maisha yako kitilie mkazo na ukifanikishe mpaka mwisho, CCM inaweza kutawala raia wajinga, ndio maana mkazo mkuu wa ccm ni raia wajinga kulindwa na kuudumisha ujinga wao.
Na Yericko Nyerere