Njaa yakimbiza wanafunzi shule

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Njaa yakimbiza wanafunzi shule

Jumla ya wanafunzi 1,368 wa shule za sekondari Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wamegundulika kuwa ni watoro kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya kukosa chakula wakiwa masomoni.

Wilaya hiyo yenye jumla ya wanafunzi 12,296 wa sekondari, inaelezwa utoro huo wa kutisha umesababishwa na mambo mbalimbali, ambapo kundi kubwa ilikitokana na ukosefu wa chakula shuleni hasa cha mchana.

Taarifa hiyo ilitolewa na Ofisa Elimu Taaluma wa Sekondari wilayani hapa, Basil Mrutu, katika kikao cha wakuu wa shule za sekondari kilichofanyika mjini Chanika mwishoni mwa wiki.

Mrutu alisema mbali ya kukosekana kwa chakula, vichocheo vingine vya utoro ni pamoja na kuwinda, kuwasaidia wazazi wao hasa mama zao kukata nyasi na makuti ya kuezekea nyumba.

Alisema sababu nyingine ni kutokana na baadhi ya wazazi kutowajali watoto kwa kufuatilia maendeleo na mwenendo wao kitaaluma na badala yake wamekuwa wakiwaacha huru na kujiamulia watakavyo.

Hata hivyo, alisema wanafunzi 15 walifariki dunia, 236 wamehama na 16 hawajulikani walipo pamoja na wazazi wao.

Alisema idara ya elimu ya sekondari wilayani hapa, imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa vijana hao waliohama wanafuatiliwa kujua kama wanaendelea na masomo huko waliko au la kutokana na kuwepo madai kwamba baadhi yao huchukua uhamisho hewa na baada ya kufanikiwa huacha masomo na kuolewa au vinginevyo.

“Tuna mikakati kuwa watoto ambao wazazi wao hawana uwezo wa kulipia ada, sare au michango mbalimbali, wafike shuleni watapokelewa na watasoma kama kawaida. Tumewasiliana na wakuu wa shule ili wawasaidie watoto hao kuwanunulia madaftari na kalamu,” alisema Mrutu na kuongeza kuwa:

"Lengo ni kuhakikisha kuwa kila mtoto aliyepata nafasi ya kujiunga sekondari anasoma bila kipingamizi chochote. Sasa kwa wale wazazi ambao watashindwa kuwafikisha watoto wao shuleni, tayari tumeanza kushirikiana na maafisa watendaji wa vijiji na kata ili wawakamate na sheria ichukue mkondo wake."

Alisema wameona mafanikio kwa Shule za Sekondari za Ndolwa, Kwedizinga na Kwaludege ambazo hutoa chakula kwa wanafunzi na kufanya vijana wapende kuhudhuria masomo yao kila siku na kukomesha utoro, ambao awali ulikuwepo katika maeneo hayo.

Ofisa huyo alisema wameanza kuwashawishi wakuu wa shule kuweka mikakati ya kuwapikia chakula watoto katika sekondari zote wilayani hapa, hasa Misima, Kwenjugo na Kwamsisi ambazo zinaongoza kwa utoro.


CHANZO: Nipashe
 
tungekuwa na namna nzuri ya kumanage resources na pesa tunazopata, hii ni kitu kidogo sana kuaddress, na watoto wetu wangeendelea na shule kama kawaida. lakini namna matumizi ya pesa yalivyo,namna wizi wa pesa ulivyo, namna mashangingi yalivyo, pesa yote inaishia kwa wakubwa, hawa wanafunzi na watu wengine wa hali ya chini wanaendelea kupata shida. ni dhambi kubwa sana kuiba pesa ambayo ingesaidia watu wengine kuinuka kimaisha, kuna watu wengine wanakufa au kupata shida kwasababu ya rushwa na wizi wa pesa za selikali ambazo zingetumika kutatua matatizo yao. kuna wengi wana njaa na selikali haitoi ruzuku ya kutosha kwaajili ya kuhamasisha kilimo na kuleta kilimo na ufugaji wa kisasa...watu wengine wanakufa hospital kwa kukosa hela ndogo tu...hela unayoiibia selikali inaleta madhara makubwa sana kwenye jamii na you will pay the price before God, hata kama mahakama za kidunia zitakushindwa.....Mungu atawatetea hao wanaolia kila siku kwasababu ya maisha magumu yaliyosababishwa na wewe uliyeiba hela ya umma....Neno Linasema, rushwa hupofusha macho, rushwa ni dhambi per se. epukeni rushwa, na ninyi mnaokula rushwa jueni kuwa mnafanya dhambi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom