Njaa mbaya sana, matapeli nao wanataka kula

Hata mie kuna mbwa mmoja alikuwa anatuma hizo sms za kijinga kila siku
 
mjibu hivi "asante sana kwa dawa yako ni kweli dawa inafanya kazi pesa zimeongezeka sana na nimeagiza Yutong zingine 13, asante sana bwana mganga"
 
bdf967bff71df13d34f5f31c3906db53.jpg
 
huyu boya mpigie atakwambia yuko sumbawanga sijui kijiji gani? baada ya kukosa kazi niliamua kumpigia

tukaongea mengi kaniuliza shida yangu...nkamwambia pesa, kiwango gani nimewahi miliki nkamwambia m10. nataka sh. ngapi nkamwambia m20-30 baada ya maongezi kanambia anaona hazitoshi atanipa 50.

wakati wote wa maongezi anakwambia hakikisha hakuna mtu maana hapendi vivuli vya watu, ikafata kumpa majina 3 ayaweke kwenye kilinge nkampa ya uwongo.

baada ya hapo nkaambiwa chukua buku 10 weka kwenye paji la uso na useme matatizo yako yoooooote ...mi namsikiliza tu .nkamwambia tayari

ananambie itume kwa mpesa ili aweze yasoma matatizo yangu akimaliza atairudisha.nikamwambia niko bush anitumie buku 5 niende town nkaitume ntamrudishia kaanza stori subiri wajukuu waje(yeye anajifanya ni babu ) waangalie kama kuna hela humu.

ikawa zamu yangu kumtwangia kila day anipe buku 5 akaishia sema hana hela mpaka auze mbuzi sijui nini nkasema bahati yako.
 
Tapeli anatuma huu ujumbe;

"Bw Jolam nashukuru kwa kunishukuru nilivyokusaidia umepata utajiri umefunguwa maduka ya jumla na umenunuwa daladala hongera kwa kufuata masharti badirisha hizo dawa kwenye magari mimi nitakuja huko bado nipo kwa mwarabu nazindika mabasi yake ila nasikitika yule ndugu yako pakomi wa bukoba nimemsaidia akiwa mbali amepata utajiri hataki kuja kunishukuru ananitumia hela tu asizani magari na majumba kafika naweza kumfilisi embu nipigie nikupe maelekezo”.

Namba inayotuma Ujumbe, 0755370384

Huu ni utapeli mwingine na ni uhalifu kama uhalifu mwingine wa kimtandao. Huyo anajifanya kakosea namba, ili ukitafakari na maisha magumu basi umpigie then unafikiri nini kitafuata...
Hata mimi nilitumiwa moja kama hii.....nilimwambia nina basi mia moja uko wapi nikupe bilioni uzindike.....hakurudi tena mpaka leo
 
Nami hii namba 0684 945 886 tangia mwaka 2015 ananisumbua tu, namtukana wala hasikii anapumzika miezi kadhaa tena ananipigia na kujiekiti kuwa ananifahamu
Anasema aniunganishe na wazungu mara tukalime huko singida mara tununue pembejeo za kilimo yaani simuelewi kabisa
 
Hii ilikuja...
MJUKUU WANGU KISINZA MBONA UJARUDI TENA KUJA KUOGA ILE DAWA NIMESHA RUDI KUTOKA KONGO NA ILE NDAGU ULIYOKUWA UNAITAKA NIMESHA KUJA NAYO KUTOKA KULE KONGO NA YALE MAGARI UNAYOENDELEA KUONGEZA KILA BAADA YA MWAKA NATAKA UYALETE HAPA NYUMBANI TUJE TUYAZINDIKE NA DAWA NI MIMI BABU YAKO MZEE KABWE. UKIPATA UJUMBE WANGU NIPINGIE
 
Tapeli anatuma huu ujumbe;

"Bw Jolam nashukuru kwa kunishukuru nilivyokusaidia umepata utajiri umefunguwa maduka ya jumla na umenunuwa daladala hongera kwa kufuata masharti badirisha hizo dawa kwenye magari mimi nitakuja huko bado nipo kwa mwarabu nazindika mabasi yake ila nasikitika yule ndugu yako pakomi wa bukoba nimemsaidia akiwa mbali amepata utajiri hataki kuja kunishukuru ananitumia hela tu asizani magari na majumba kafika naweza kumfilisi embu nipigie nikupe maelekezo”.

Namba inayotuma Ujumbe, 0755370384

Huu ni utapeli mwingine na ni uhalifu kama uhalifu mwingine wa kimtandao. Huyo anajifanya kakosea namba, ili ukitafakari na maisha magumu basi umpigie then unafikiri nini kitafuata...
Mimi nilishatumiwa sms hiyo japo namba tofauti nlipompigia akanifanya alikosea namba nikaomba kuonana nae ili anifanyie "settings" hii biashara yangu ya "Vitanda vya jumla" a.k.a (majeneza) iende vizuri nipate wateja wengi matajiri hasa wabunge na mawaziri maana hao ndio hununua majeneza classic.
Lakini huyo mganga alipoanza kuomba nimtumie hela nikaona ni tapeli tu.!
 
mara nyingi ikiibwa cm,lain inatupwa sasa hawa watu wakiipata lain yako hauna bahati.wanatarget namba muhimu kama mama,baba,dada,mjomba,baby,my luv.kisha wanatumia ujumbe wakijifanya ni wewe muibiwa cm na kuomba hela.ukipiga awapokei eti utume text.ukijitusu tu umeumia.hushangai namba yako wanatoa wapi?
 
Back
Top Bottom