Njaa mbaya sana, matapeli nao wanataka kula

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Nov 7, 2012
1,976
3,127
Tapeli anatuma huu ujumbe;

"Bw Jolam nashukuru kwa kunishukuru nilivyokusaidia umepata utajiri umefunguwa maduka ya jumla na umenunuwa daladala hongera kwa kufuata masharti badirisha hizo dawa kwenye magari mimi nitakuja huko bado nipo kwa mwarabu nazindika mabasi yake ila nasikitika yule ndugu yako pakomi wa bukoba nimemsaidia akiwa mbali amepata utajiri hataki kuja kunishukuru ananitumia hela tu asizani magari na majumba kafika naweza kumfilisi embu nipigie nikupe maelekezo”.

Namba inayotuma Ujumbe, 0755370384

Huu ni utapeli mwingine na ni uhalifu kama uhalifu mwingine wa kimtandao. Huyo anajifanya kakosea namba, ili ukitafakari na maisha magumu basi umpigie then unafikiri nini kitafuata...
 
Matapeli wa vijijini hao, maaana mimi unitumie sms kama hiyo wakati hata baiskeli tu mfupa wa mbwa sina si
ntakuona punguan waheed.
Tapeli anatuma huu ujumbe;

"Bw Jolam nashukuru kwa kunishukuru nilivyokusaidia umepata utajiri umefunguwa maduka ya jumla na umenunuwa daladala hongera kwa kufuata masharti badirisha hizo dawa kwenye magari mimi nitakuja huko bado nipo kwa mwarabu nazindika mabasi yake ila nasikitika yule ndugu yako pakomi wa bukoba nimemsaidia akiwa mbali amepata utajiri hataki kuja kunishukuru ananitumia hela tu asizani magari na majumba kafika naweza kumfilisi embu nipigie nikupe maelekezo”.

Namba inayotuma Ujumbe, 0755370384

Huu ni utapeli mwingine na ni uhalifu kama uhalifu mwingine wa kimtandao. Huyo anajifanya kakosea namba, ili ukitafakari na maisha magumu basi umpigie then unafikiri nini kitafuata...
 
Jinsi maisha yanavyozidi kutaiti ndivyo na akili zinazidi kupevuka,Lakini hapo pamoja na maisha kuwa magumu lakini kuna watu watapigwa tu
 
Niliiona hii meseji kwenye simu yangu ila sikuhangaika nayo nikawa na subiri anipigie ngoja leo nimtwangie mimi.
 
Hizo SMS huwa na-futa kabisaa tena fastaa ili nisijaribu hata hiyo kupiga hiyo namba
 
Wanaopenda ushirikina na uchawi ndio watatapeliwa,basi waache watapeliwe
 
duuu mi juzi kati iliingia sms eti umekuwa ukihangaika siku nyingi kumtafutia kijana wako nafas za jeshi hivyo nafasi imepatikan ya kijana wako sasa nikijiangalia hapa nilipo mi ndo kijana mwenywe nilimjibu tu kuwa huwezi nitapeli kirahis hivyo tangu siku hyo hakunitumia tena ujumbe wowote so tuwe makini na hawa watu
 
Back
Top Bottom