kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,872
Kumesikika malumbano kati ya serikali na wananchi juu ya hali ilyopo nchini kuhusu chakula, serikali ikisema hakuna baa la njaa huku wengine wakisema baa la njaa lipo tena huenda ni kubwa sana. Wote nadhani wanazungumuza kitu kimoja kwa mitazamo na maneno tofauti. Serikali haitaki kabisa kusikia neno kuna baa la njaa, hiyo si shida ila shida lipo kwenye tafsiri ya neno baa. kwangu mimi najua baa kama janga yaani hali isiyo ya kawaida na yenye kuhatarisha hali ya maisha.
Nikiwa najaribu kutafakari naona kilichopo nchini kuhusu chakula ni upungufu mkubwa wa chakula hasa kwa baadhi ya mikoa kutokana na ukosefu wa mvua. Mikoa ya kanda ya ziwa ikiwa ni miongoni mwa mikoa yenye hali mbaya. Kutokana na upungufu mkubwa wa chakula uliotokana na kukauka kwa mazao shambani, kukosekana kwa shughuli mbadala wa wakulima inayoweza kuwapatia pesa na hasa katika mikoa ya kanda ya ziwa watu hawana uwezo wa kumudu gharama za kununua chakula. Kwa mfano huko Rorya ambako hali ni mbaya na kulingana na waziri wa chakula na mifugo gunia moja la mahindi ni sh 150000 si kwamba ukienda kwenye masoko kama utegi, randa, ochuna, kuruya, nyamaguku,shirati, kitembe au hata tarime utakosa mahindi hapana mahindi yapo shida ni kwamba bei ni kubwa sana kiasi kwamba wananchi wanashindwa kutokana na ukosefu wa kipato kingine nje ya kilimo iliyoathirika na jua.
Wilaya zenye hali ya hewa kama Rorya zinahitaji kuangaliwa kwa karibu kuondoa njaa maana hata watu wakilima kiasi gani jua likipiga wiki moja tu mazao hukauka upesi sana.
Ni vyema wananchi popote Tanzania wakaelimishwa juu ya fursa zingine zinazopatikana katika maeno yao ili kuacha kutegemea kilimo tu. Mfano huko Rorya kuna ziwa (victoria) lakini watu kwenye tarafa kama GIRANGO, SUBA NA LUO IMBO hawapendi sana shughuli za uvuvi (wamejikita kwenye kilimo tena cha mahitaji ya nyumbani) na hata wanaopakana na ziwa pia hawalimi sana wao ni uvuvi tu, sasa wilaya nzima wananchi wanategemea ama kilimo kwa walio wengi na uvuvi kwa walio wachache. Hali hii husababisha hali ya wananchi kuwa ngumu sana kiuchumi wakati kama huu. Nashauri haya yafuatayo kufanywa huko Rorya kwa ushirikiano wa mbunge, halmashauri na wananchi.
1. Wananchi waelezwe fursa zilizopo tofauti na kilimo na ufugaji, mfano biashara inaweza kufanywa kwa uzuri kati ya wilaya hii na tarime, musoma na hata nchi jirani ya kenya.
2. Wananchi wapewe elimu juu ya uvuvi katika tarafa zote na mbunge badala ya kugawa ng'ombe za kuchinja kwenye misiba atumie hizo hela , hela za jimbo na makusanyo ya halmashauri kuwapa wananchi zana bora za uvuvi kwenye vikundi vilivyorasimishwa (kama havipo avianzishe na kuvirasisimisha).
3. Wananchi wapewe somo juu ya mazao mbadala badala ya mahindi na mihogo. Kwanza mihogo ishafeli baada ya ardhi kuchoka na mahindi pia imefeli kutokana na kukauka haraka kwa udongo.
4. Elimu ya ufundi ni muhimu sana ili kuchochea ubunifu na kuongeza pato la wananchi. Ndg mbunge badala ya kugawa pesa kwenye misiba wakusanye vijana wanaofanya ufundi kama useremala, ujenzi na wanaoshona chereheni uwasaidie kupata mkopo ili kuwainua kiuchumi .
5. Elimu juu ya utunzaji wa mazingira ni muhimu sana, nadhani hii ni moja ya wilaya zinazoongoza kwa uharibifu wa mazingira. Miti imekatwa vibaya sana kiasi kwamba hakuna hata mtu wa kujinga jua porini, mfano maeneo kama farm (Pale koryo) , watu wamelima kwenye mito na vijito mpaka kumeziba kabisa.
6. Mwisho wananchi waelimishwe juu ya kupanda miti ya matunda, yaani Rorya unaweza kutembea kijiji kizima ukapata mti wa maembe, michungwa kwenye miji 3 kati ya 20. Huwezi kuta parachichi wala mpapai na iliyopo haitunzwi. Wananchi wameathiriwa na ulaji wa ughali mpaka wanashindwa kuthamini mazao mengine.
MADIWANI, MBUNGE NA HALMASHAURI HEBU FANYENI KAZI KUBADILI HII HALI NI AIBU SANA MWANAUME WA MARA KULIA NJAA NI AIBU MNO.