Incredible
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,031
- 1,603
Leo nimesoma kwenye gazeti la Nipashe Kitila Mkumbo akitetea rais alivyoingiza msimamo wa CCM siku alipozindua Bunge La Katiba. Nipashe limeandika hivi:
Dk. Mkumbo alisema anaunga mkono hatua ya Rais KIkwete kubainisha bungeni msimamo wake juu ya mchakato huo, hasa katika suala la aina ya mfumo wa muungano wa serikali mbili au tatu.
Alisema Kikwete angekuwa Rais wa kwanza wa ajabu duniani kama asingeonyesha msimamo wake na kwamba, pamoja na masuala mengine, huo ndiyo unaotakiwa kujadiliwa na kutumia nguvu za hoja kuonyesha udhaifu wake.
"Wamkosoe au wamuunge mkono kwa hoja, Bunge liendelee lakini kwa sasa wengi wana mihemuko ya uchaguzi mkuu ujao, Bunge hili liahirishwe ili Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liendelee na lifanyie marekebisho Sheria ya Mabadiliko ya Katiba," alisema Dk. Mkumbo.
Sasa hawa wasomi wetu wanaelekea wapi? JK mwenyewe alijua na anajua kwamba amekosea. Sasa huyu msomi wetu anataka apate utajiri kwa kulamba watu miguu, atafanikiwa kweli?