Nizar uso kwa uso na Man City

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Nizar Khalfan ataiongoza timu yake ya Vancouver Whitecaps itakapoikabiri Manchester City kwenye mchezo wa kirafiki hapoJulai 18.

Khalfan ambaye amefanikiwa kujitegenezea namba ya kudumu kwenye kikosi cha Whitecaps kinachoshiriki Ligi Kuu ya Marekani MLS atakuwa ni miongoni mwa nyota watawavaa vijana hao wa Robert Mancini.

"Itakuwa ni mechi ya kipekee kucheza dhidi ya timu inayoshiriki Ligi Kuu ya England, Manchester City FC kwenye Uwanja wa Empire,î alisema Paul Barber, mkurugenzi mkuu waWhitecaps FC. "Mwenendo wetu msimu huu kwenye MLS ni mzuri sana, hivi karibuni tumefanikiwa kuvutia mashabiki wengi zaidi katika mechi zetu tatu za nyumbani.

Wakiwa na nyota wa zamani wa Italia, Mancini, Manchester City wameshatangaza baadhi ya nyota wanaoweza kuwepo kwenye mchezo huo kuwa ni wachezaji saba wa kimataifa wa England, akiwemo Gareth Barry, Joe Hart, na Shaun Wright-Phillips.

Nyota wengine ni Jerome Boateng, Nigel de Jong, ndugu Kolo na Yaya Toure, mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli, David Silva, Patrick Viera, huku Silva na Viera wote walishatwaa Kombe la Dunia.

ìVancouver ni mji wa watu wanaopenda soka na kikosi chao ni kipya kwenye MLS. Tuna historia ya kucheza na Whitecaps, tulicheza nao mwaka1980 na 1981kwenye Uwanja Empire," alisema Garry Cook, Mkurugenzi wa Manchester City FC. "Walishinda mechi zote kwa ushindi mkubwa, hivyo tunaahidi itakuwa mechi ya aina yake.î

Hiyo itakuwa mechi yao ya tatu kucheza baina yao, katika michezo miwili ya awali Vancouver ilishinda, 5-0 mwaka 1980, 2-0 mwaka 1981.

Manchester City kwa sasa ipo nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu ya England pointi mbili zaidi kwa Chelsea. Kama wataendelea kuilinda nafasi hiyo watafuzu moja kwa moja kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa.
 
Watafuzuje wakati LIVERPOOL FOOTBALL CLUB ndiyo hivyo wamekumbuka shuka ingali kumekucha. Nafasi ya 4 ni ya hao mabingwa wa zamani.
 
all the best NIZAR tngependa tkuone ukifika mbali zaidi ya hapo ili uwe mfano kwa wabongo wenzako...
 
Mbona unachanganya mambo mkuu. Nizar anacheza timu ya Canada. Sio MLS .
 
Back
Top Bottom