Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,291
- 2,466
Kosa kubwa sana analofanya huyu producer anayeitwa Rioba ambaye alikuwa ni meneja wa Young D. Nimegundua ni kwa nini hawa watu hawakaki pamoja kikazi kwa muda mrefu na baada ya muda wanatibuana.
Nimemsikia jana kupitia FNL. Huwa nafuatilia humo mara moja moja hasa nikiona Kipimajoto cha ITV kinaniboa (ila cha jana kilikuwa poa). Sasa huyu 'Luciuos Lyon' wa bongo anavyoonekana anataka kujenga matarajio makubwa sana kwa msanii anayemmiliki, kiasi cha kufikia kuonekana kumghasi msanii. Kumghasi kwa maana ya kutaka kuingilia kila jambo la msanii pamoja na kuweka 'ubaba' mwingi kiasi cha msanii kuona anakosa uhuru. Angeweza tu pia kumruhusu Young D kuishi anapopenda yeye na si lazima chini ya himaya ya meneja.
Hata ikitokea anakuwa na msanii mwingine chini yake yatatokea haya haya. Rioba akiweza kugundua udhaifu wake ndipo ataweza kufanya kazi na msanii. Nilivyosikia tu habari za Empire ndio nikajua kuwa pana tatizo hapo. Kuwa wewe, Bro! Huwezi kuwa Lucious Lyon. Hata Empire haikukupa somo jinsi jamaa alivyoishia kuvurugana na wanawe. Wala huyo Young D hawezi kuwa Hakeem ambaye naye alikuwa ni msanii tu katika filamu na si msanii katika muziki. Ni hayo tu kwa sasa