Misunderstood
JF-Expert Member
- Aug 4, 2020
- 392
- 896
Mkurya mkuu
Ushauri wako umenibariki sana. Mtoto wa kwanza ana vita sanaMtoto wa kwanza ana vita kubwa sana ya kiroho ila kwa leo sitozungumzia hilo....ila Shetani anapenda kuwaharibia future sana watoto wa kwanza kwa kuwa anajua kwamba mtoto wa kwanza akifanikiwa basi kwa wanaofuata huwa ni rahisi....Lichunguze hilo....Nimesema hivyo kumaanisha kuwa wewe ndie umebahatika na unaeweza kurejesha amani tena kwenye familia hivyo Focus kutengeneza maisha yako kwanza huku ukimuomba MUNGU akuongoze utimize hilo kwa haraka then ndio uangalie utaratibu wa kutengeneza ya hao wa nyuma yako....Hapo ukicheza vibaya mtajikuta level moja japo unasema una elimu maana hiyo vita ni ya Shetani
Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna 'Mkurya' Mjivuni ( Majipu ) na Mshamba ( Mbwiga ) hivyo Mkuu. Huyo nahisi atakuwa ni ama Mhaya au Mjita na pengine akawa ni Mjaluo.
You are welcomeUshauri wako umenibariki sana. Mtoto wa kwanza ana vita sana
Achana nae huyo wala usingemjibuKama sijakuelewa kaka! Kwamba nimejivuna au? Hali yoyote niliyoielezea hapo ni ili tu mpate picha halisi ilivyo ningeficha vingine cdhani kama ningeeleweka! Na wala sina majivuno kabisa! Km nimekukwaza pole
Usi hangaike kumjibu uyu Popoma atakupotezea mda wakoKama sijakuelewa kaka! Kwamba nimejivuna au? Hali yoyote niliyoielezea hapo ni ili tu mpate picha halisi ilivyo ningeficha vingine cdhani kama ningeeleweka! Na wala sina majivuno kabisa! Km nimekukwaza pole
.... Pole sana bila shaka unamoyo wa upendo kwandugu zako huko kwenu kskazini mnatabia za kukaa na wamama Nawababa nyumbani mnawaita watoto bado sisihuku kwetu kusini ukisha barehe unaonyeshwa kaeneona myanzi ilipo hapo umeazimwa ukimaliza shule hakuna was kukupa mtaji utajiongeza mwenyewe mambo yakianza kuku bana hakuna wakukupa sabuni wars shati wala wala jembe na baba akijua umekua huwa anaanza ulinzi kwenyeshamba lake LA kokoa hataki utani.hapo anakupiga tumajungu utaskia araa umekuwa mwanangu naona ndevu zimekuwa kama nywele"afu uko piii. Owa bwana.utakapo mwamvia baba sins Hera ndo anakupa makavu hapo hapo kwamba hapo unapo kaa nikwangu tafuta Hera ununue pakwako.kuanzia Leo noskuone unakuja kuvonge ugali humu huu ugali wakwangu Mimi na nama yako full stop."" Sasa hapo mtoto wakiume unaanza kujiuliza hivi yule lama niliye soma nae yukowapi?? Basis utapambana utajua yuko wapo mishegani kama madini mkokoteni nk unajichanganya huko mungu anabaliki unapata michongo maisha yanaenda. Kwahiyo kumsaidia saana MTU wakatimwingine unamhalibu punguza kiwango chamboga punguza shobo nao watajiongeza wenyewe unajua motto wakiume niwakiumetu ataondoka kwa kukuchukia akifanikiwa ataludi nakitenge na ahsante nhingiHabari zenu ndugu zangu!
Mimi ni mdada at my early 20’s. Na ni mtoto wa mwisho na wa kike katika familia yetu nikiwa na kaka zangu wawili mmoja early 30’s mwingine late 20’s. Katika familia yetu mimi ndiye niliyefanikiwa kufika hadi degree nawashukuru wazazi wangu waliweza kunipigania na juhudi zangu pia. Ila kaka zangu mmoja alifanikiwa kufika diploma tu.
Familia yetu ilipitia changamoto nyingi sana sana za kuumiza lakini nashukuru Mungu tupo hai mpaka sasa. Na Mungu kanijalia kazi nzuri, ninajitegemea na kusaidia ndugu zangu pale niwezapo. Nilianza kazi mwaka jana mwezi wa Tano, nikasave nikafanikiwa kununua kiwanja na kufikia hadi hatua ya kuweka msingi! Niliamua kufanya hivyo kwasababu familia yetu hatujawahi kuwa na nyumba yetu wenyewe ya kumiliki! Kwahiyo ni kitu kilichokuwa kinanipa wasiwasi sana vipi siku kikitokea cha kutokea tutaenda wapi? Hivyo nikalipa lengo langu hilo priority.
Lakini sasa kaka zangu bado wanabangaiza vibarua walivyo navyo vinawasaidia kula na nauli za kwenda vibaruani na mara nyingine hata inanibidi niwape mimi hata hela ya nauli na ya kula! Na ilifika kipindi cha kulipa kodi basi nitoe yote au niwachangie! Hili sio tatizo maana najua Mungu kanipa uwezo ili niwasaidie ndugu zangu.
Swali ni ‘niwasaidiaje kakazangu?’ ili waweze kusimama vizuri kiuchumi? Maana mmoja tulishawahi kumchangia mtaji lakini biashra ikawa ngumu ikafeli. Mwingine hana passion na biashra na haiwezi tu niseme ila kibarua chake ni cha kipato kidogo sana. Wanashindwa hata kuoa kwasababu hawako vizuri kiuchumi. Kiukweli naumiaga sana na ni kama inaniongezea depression nikiwafikiria! Kuna wakati nakwama lakini najua sina ndugu wa kumuomba msaada naumia sana!
Sasa naomba mnisaidie ushauri na maoni, niwasaidieje? Je, ina maana mimi kuendelea na ujenzi ilihali ndugu zangu hawako vizuri kiuchumi? Natamani nichukue mkopo niwape kwaajili ya biashara lakini vipi zikifeli maana tayari ilishafeli! Je, ni sawa kuwawazia sana?
Samahani kwa kuwachosha! Natanguliza shukrani.