Niulize maswali kuhusu Sonography

Mr DIY

JF-Expert Member
Dec 24, 2016
1,111
2,320
Mwenye shida au kutaka uelewa kidogo kuhusu hii professional karibuni kwa maswali

IMG_20201216_112341_419.jpg
 
Nini maana ya sonography?

NB. Tumia kiswahili
Kiswahili kigumu ila nitajitahidi, sono ni sauti so ni matumizi ya sauti hasa sauti iliyo na frequency juu ya uwezo wa binadamu kusikia (ultrasound) ili kuweza kuona viungo vya ndani ya binadamu, professional wake anaitwa Sonographer. Japo wengi mtaani tunaita ultrasound au wengine wanaita picha.
 
Naweza kufanya sonography ya meno? Nataka kujua mizizi ya meno yangu iko umbali gani sitaki kupiga xray.
 
Hiyo mashine ina madhara yoyote ukitumia mara kwa mara?
Hakuna limitation ya kutumia sauti katika uchunguzi, na hakuna ushahidi wa madhara ya sauti katika mwili sababu sauti hubeba energy kidogo si rahisi kufanya uharibifu na kubadili mienendo ya seli kama mionzi mingine inavyofanya, mfano kuna wanyama wengi wanatumia sauti ku navigate mfano popo
 
Naweza kufanya sonography ya meno? Nataka kujua mizizi ya meno yangu iko umbali gani sitaki kupiga xray.
Hapana si rahisi kutumia sauti kwenye uchunguzi wa meno, sauti haipenyi kirahisi kwenye tissue za meno hivyo hutopata matokeo mazuri kama ukitumia x-rays
 
Hapana si rahisi kutumia sauti kwenye uchunguzi wa meno, sauti haipenyi kirahisi kwenye tissue za meno hivyo hutopata matokeo mazuri kama ukitumia x-rays
ni magonjwa ya aina gani yanatakiwa kufanya hiki kipimo? ukiacha wamama wajawazito?
 
Muda wowote daktari atataka fahamu au jiridhisha na mafikirio ya tatizo la mgonjwa
 
Mkubwa hiyo teknolojia ina matokeo kiasi gani kwenye kupima tezidume
Tunaitumia katika hatua za awali kujua ujazo au ukubwa wa tezi dume pia baadhi ya dalili za kansa kwenye tezi dume pia inatumika kuonesha njia wakati wa kuchukua sample ya kinyama ili kwenda pima hiyo tezi dume
 
Upo vizuri Mtaalamu!
Swali; Ultrasound inaweza kuonyesha vidonda vya tumbo?
 
ni magonjwa ya aina gani yanatakiwa kufanya hiki kipimo? ukiacha wamama wajawazito?
Kuna vipimo vingi waweza pia baadhi ambavyo ni common ni vifuatavyo

abdominal ultrasound-hapa ni tumbo kiujumla

Pelvic uss- hapa ni chini ya kitovu hasa mifumo ya mkojo na kizazi

Gynacological uss-hapa tuna deal na viungo vya uzazi kwa mwanamke

Obstrectic uss- hapa ni assessment za mimba

Cranial uss-hii ni kwa ubongo hasa watoto wachanga

Occular uss- hapa ni jicho

Neck uss- hapa ni kwaajili ya tezi ya thyroid iliyopo shingoni

Breast uss-hii hufanyika kwenye matiti

Echo cardiogram uss-hii inapima uwezo wa moyo

Scrotal uss-korodani zinapimwa

Kub/ruv uss-hizi zinafanyika kwa assesment za mifumo ya mkojo pamoja na uwezo wa kibofu na tezi dume kuhimili mkojo

Superficial uss-hii tunaifanya kwenye ngozi inategemea na shida ya mgonjwa mf uvimbe wa hernia

Doppler uss-hii tunaifanya kwenye mishipa ya damu kujua uwezo wake kuhimili damu pia tunajua flow ya damu ili kuhudumia sehemu mbali mbali za mwili.

Hizo ni baadhi tu ya test za ultrasound ambazo tunafanya hapa Tanzania. Hii carrier ni pana sana sana japo hapa kwetu haijatanuka sana sababu kuna wataalamu wachache na vifaa duni, mashine iliyoshiba ya ultrasound inauzwa zaidi ya milioni 200. Zingatia kuwa aina hizo juu za vipimo zitatofautiana sehemu moja na nyingine sababu kuu huwa mbili kwanza sonographer mwenyewe itategemeana amefundishwa hasa aina gani ya kipimo mfano echo cardiogram mara nyingi hufanya na Radiologist pia aina ya mashine na uwezo wake sio kila mashine inaweza fanya kila kitu inategemea na software iliyomo na hardware zilizopo ku upgrade hizi kitu ni gharama mno aisee
 
Upo vizuri Mtaalamu!
Swali; Ultrasound inaweza kuonyesha vidonda vya tumbo?
Jibu ni hapana, usije danganywa vipimo ambavyo unaweza pima vidonda vya tumbo kwanza Dr anaweza kukusikiliza na kukuuliza baadhi ya maswali akakuhisia una vidonda vya tumbo pili kuna aina ya x-ray inaitwa Barrium meal swallow x-ray. Cha tatu ambacho ni uhakika kinaitwa OGD kwa kifupi, hichi uhakika wake ni 100%
 
Ahsantee
 
Back
Top Bottom