Niulize chochote kuhusu tiba ya mionzi

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,662
Habarini....Kwasasa kuhusu Tiba...Mambo yamebadirika....Clinical Medicine inaanza kupotea kwa Kasi na Clinical Imaging inakuja kwa kasi sanaa...!!! Hapa naamanisha kuwa Ukienda hospitalini vipimo vingi wasipo kwambia Maabara basi watakutaka uende Radiology Department! Madaktari siku hizi hawataki kuumiza kichwa...Wanakambia kwenye Medical Imaging na kwao inakuwa rahisi kuamua Nini cha kufanya!

Medical Imaging inahusisha...Vitu vifuatavyo nitaichambua kifupi sana lakini kupitia maswali yenu ndio tutapata vitu vingi zaidi

1)PLAIN X-RAY-Hii ni common sana sehemu nyingi na vitu vitakavyo pelekea wewe kufanya Plain X-Ray ni kama Ajari labda umevunjika mguu,kiuno au kitu chochote katika mwili hii itasaidia kuonesha tatizo kwa haraka,Mtoto kumeza sarafu,matatizo ya kifua ambapo Chest X-Ray ndio common Sanaa! Kukabwa na mfupa,mtu akipigwa risasi kama imebaki mwilini,matatizo ya uzazi na mengine mengi itategemea na Daktari amekuandikia nini

......Ndani ya Plain X-Ray kuna Vipimo special ambavyo vinaweza kufanyika kama barium swallow,Barium Enema,Barium Meal,HSG,IVU kuangalia Figo! Na vingine vingi

2)ULTRASOUND-Hii pia hufanyika hasa kwa kina Mama wenye mimba,Matatizo ya uzazi,au matatizo mengine yoyote kwa mtu yoyote yanaweza kufanyika kama kuangalia mishipa ya Damu,vitu vyote vilivyopo tumboni na matatizo mengine

3)CT SCAN-Hii inafanya vitu vyote vinavyo fanywa na PLAIN X-RAY na ultrasound ila inavitu vingine vya ziadaaa na vingi!!!

4)MRI-Hii pia unaweza kuangalia vitu vinavyo fanywa na CT scan....Hasa soft tissue

5)MAMOGRAPHY-hii kwa wanawake kuangalia Matiti

6)Nuclear Medicine-Hapa bongo Haipo

Sasa hapo juu nimeelezea kwa juu juu sana sababu inavitu vingi sanaaaaa!! Niulize chochote nitakusaidia kukuelekeza....Kuanzia

1)MAANDALIZI
2)GHARAMA
3)UMUHIMU
4)JINSI KIPIMO KINAVYO FANYIKA
5)TOFAUTI ZAKE

Hapa mimi nitakuelekeza kadri ya uelewa wangu japo nikupe mwanga wa nini kinaenda kufanyika...utajisikiaje na ushauri mwingine wowote unao husu hivi vipimo!

Sidhani kama hospital au doctor huwa anakuelezea itakavyo kuwa!

Na wengi wamekuwa na imani potofu kuhusu hivi vipimo lakini hapa tutaelimishana!!

Japo upate mwanga kabla ya kufanya kipimo

Kumbuka Vipimo hivi vinaweza kufanyika sehemu yoyote ile ambayo vipo! Na wajuzi wengine mtasaidia kujibu maswali

Karibuni
 
Ahsante mkuu!
Swali langu ni kuhusu madhara ya hizi mashine za mionzi, je zina madhara kwa mtu anayefanyiwa kipimo ? ni yapi....ukinijibu nakuja na maswali mengine...
 
Madhara inategemea na unafanyiwa kipimo cha nini....Kama Ni plain x-ray,CT SCAN,MRI,ULTRASOUND,AU MAMOGRAPHY....

Lakini swali lako kama sijakosea nadhani unaongelea kuhusu Mionzi! Ukweli ni kwamba Mashine hiz zinatoa Mioni lakini madhara yake ni madogo kuliko Faida utakayo ipata! LABDA nikqambie kuwa ULTRASOUND HAINA MIONZI SO hio kwenye Suala la mionzi itoe haina effect! Pia MRI nayo haina madhara ya mionzi kwasababu haitumii mionzi ila madhara mengine yanaweza kutokea sio wote wanapatwa kwa Ultrasound na MRI

Tukija kwenye Plain X ray na CT na Mamography ....hizi zinatumia mionzi kutengeneza Image...Sasa hapo tutaangalia Effect ya Mionzi japo sio kwa kiasi kikubwa na ni madhara ya baadae sana ambayo ni probability kupata.....Cell zinaweza kufa,unaweza kupata cancer lakini sio kwamba ukifanya lazima utapata hapanaa.....Hizo ni Risk Factors

Ndio maana Daktari anashauriwa Kuangalia madhara ya hizi mashine wakati anachagua kipimo mfano kama ana uhakika kitu kinaweza onekana kwenye PLAIN X-RAY hana sababu ya kusema ukafanye CT scana kwasababu CT scan kwa upande wa Dozi ya mionzi ina Dozi kubwa kuliko Plain X-Ray.....MFANO DOSE ANAYO PATA mtu anae pima CT scan ya kichwa ni Sawa na mtu Alie fanya plain Chest X -ray (kifua) 400-500 lakini haimanishi kuwa atapata Madhara hapo anaweza pata au asipate.....Hadi sasa sijapata kuona kama Kuna mtu alipata Madhara ya mionzi baada ya kupimwa labda nikimaliza Research yangu juu ya hili nitakuwa na majibu kamili

Lakini hadi sasa FAIDA zake ni kubwa kuliko Madhara

Karibu kama hujaelewa sehemu
 
Hapa patamu sanaaaa

Mie ningependa kuanzia kwa kujua wastani wa cost za kila kipimo in TZ

Pili hapa Tz kuna watu special wanaosomea radiology or maana nimezoea kuona ma Dactari huko mahospitalini kujihusisha, hasa kusoma majibu ambayo smtyms huwa yanawazingua sanaaa.
 
Mkuu nna mdogo wangu anasumbuliwa na kifua, akipumua hua kinamuuma kwandani, anasema kinamuuma sana mpaka anatamani kupiga kelele.
Tumejaribu kumpeleka hospitali kwa kufanyiwa vipimo vya kawaida na kupatiwa dawa ila bado haijasaidia. Sasa tumekata shauri kesho tunataka tumpeleke akafanye moja kati ya hivo vipimo..
Swali langu, ipi kati ya hivo vipimo ni bora tuende tukafanye (zingatia na gharama)
 
Cost itategemea na Hospital lakini kiuhalisia ni kuwa Hospital za Private zina gharama kubwa katika hivi vipimo kuliko hospital za Serikali....Mfano umeandikiwa CT scan ya Kichwa Muhimbili ni laki na nusu kwa laki mbili na nusu wakati hospital zingine ni hadi laki 5 au 6

Kusoma picha anae ruhusiwa ni Radiologist yaani kasoma MEDICINE MIAKA 5 then Akaja kuspecilize miaka 3! Raiographer ndio mwenye ruhusa ya kufanya hivi vipimo na si mwingine yoyote iwe radiologist au medical Doctor....Radiographer anaruhusiwa kuandika report ya Uktrasound tuu japo vipimo vingine vyote anaweza Kukwambia shida yakoo maana anajua ila haruhusiwi.....na sasa mjadala mkubwa ni kumtaka Radiographer kuruhusiwa kumpa mgonjwa report i mean kusoma!!! Kuna conference nilihudhuria wana mpango huo!!

Japo daktari wa kawaida anajua baadhi ya vitu katika picha ila yeye atasubiri report tuu anaweza kukwambia lakini sio in details
 
Mkuu nna mdogo wangu anasumbuliwa na kifua, akipumua hua kinamuuma kwandani, anasema kinamuuma sana mpaka anatamani kupiga kelele.
Tumejaribu kumpeleka hospitali kwa kufanyiwa vipimo vya kawaida na kupatiwa dawa ila bado haijasaidia. Sasa tumekata shauri kesho tunataka tumpeleke akafanye moja kati ya hivo vipimo..
Swali langu, ipi kati ya hivo vipimo ni bora tuende tukafanye (zingatia na gharama)
Matatizo ya kifua mara nyingi mgonjwa huanzia Plain X-ray na baadae daktari hushauri CT SCAN.... Pia daktari anaweza kuorder moja kwa moja CT SCAN

Gharama ni kuwa CT scan ni gharama kuliko Plain X-ray....CT scan ni laki moja na Nusu kwa laki 2 na nusu hospital za serikali wakati Chest X-ray ni Elfu 15 hadi elfu 18

Ila CT IS THE BEST kuliko Plain X ray.....
 
Mie nahitaji kufahamu tuu hiki kipimo kinaitwa "Laparoscopy " kinahusika hasa ktk kutambua maradhi gani.?
Hii ni procedure yaani ni upasuaji (mdogo sana) yaani small incision ambao unahusisha Tube nyepesi na nyembamba hasa kuangalia organs za zilizopo kwenye Tumbo au pia kwa wanawake....inaweza kutafuta viumbe vidogo vidogo...infections

Ni sawa na Laparatomy ila tofauti ni kuwa hii laparoscopy inatumia tube nyembamba na nyepesi tofauti na laparotomy ambayo inatumia large incision wakati laparoscopy ni small incision
 
Matatizo ya kifua mara nyingi mgonjwa huanzia Plain X-ray na baadae daktari hushauri CT SCAN.... Pia daktari anaweza kuorder moja kwa moja CT SCAN

Gharama ni kuwa CT scan ni gharama kuliko Plain X-ray....CT scan ni laki moja na Nusu kwa laki 2 na nusu hospital za serikali wakati Chest X-ray ni Elfu 15 hadi elfu 18

Ila CT IS THE BEST kuliko Plain X ray.....
Shukran mkuu
 
Mionzi ya tiba inatofautiana nini na mionzi ya kwenye microwave?
Mionzi ya Tiba unamaanisha ile ya Radiation therapy au

Ila kwa modalities nilizo taja hapo juu ni kuwa Microwaves na X-rays zinatofautiana kwenye wavelengths na frequencies

Microwaves zipo katikati ya infrared radiation na juu ya radarradiation wakati X-rays zipo katikati ya ultraviolet radiation na chini ya gamma ray radiation.
 
Je ,ultrasound inaweza ikaonesha uvimbe kama mtoto na mtoto kama uvimbe hali ya kua mtoto amefikia miezi zaidi ya 6 akiwa tumboni kwa mama yake?
Hapana Haiwezekani ila mtoto wa miezi sita alie tumboni kama ana uvimbe utaonekana.....haita onesha kama mtoto kama uvimbe kwa sababu mtoto akiwa tumboni na mama akienda kufanyiwa ultrasound huwa wanaangali kama mapigo ya moyo ya mtoto yapo sawa na vitu vingine......Japo misdiagnosis hutokea lakini sio kama ulivyo sema
 
Mionzi ya Tiba unamaanisha ile ya Radiation therapy au

Ila kwa modalities nilizo taja hapo juu ni kuwa Microwaves na X-rays zinatofautiana kwenye wavelengths na frequencies

Microwaves zipo katikati ya infrared radiation na juu ya radarradiation wakati X-rays zipo katikati ya ultraviolet radiation na chini ya gamma ray radiation.

kadri unavyotujibu maswali yanaibuka mengine..
Je mionzi ya microwave ina madhara gani? je yale majiko ya kupashia ya microwave hayana madhara kwenye chakula tunachokiweka humo? maana nasikia kutoka kwa wataalamu wa tiba asili husema chakula kinapoweka kwenye microwave huharibika nutrients zilizomo kwenye chakula, hivyo tusitumie hizo majiko

Kuna madini huwa yanatoa mionzi kama Uranium tena mionzi yake kwenye mitambo inayotumia hiyo nishati hulindwa sana isipatikane leakage...je tofauti ya mionzi hiyo ni nini?
Kuna mionzi nasikia ya gamma rays na beta rays na x rays je kati ya hiyo ni ipi ina madhara, na mashine hizi hutumia mionzi gani kati ya hiyo?
 
Kwa upande wa Microwave sijajua ila nacho jua kuwa microwave inashort wavelenghts means Energy yake ni ndogo na risk ya scatter radiation ni ndogo..so kwa uapnde wa mdhara ni kidogo sana Kuliko mionzi tunayo ipata sehemu nyingine

Kuhusu kuhifadhi chakula nacho jua ni kuwa artifical methods zote za kuhifadhi chakula zinapunguza ubora wa chakula kama Friji na vitu vingine Japo Am Not sure 100%

(WATAALAMU WATATUSAIDIA HAPO)

Kuhusu Gamma Rays,X-rays na beta Rays kuna tofauti kwenye uwezo wa kupenya....nguvu zake na Wavelengths.....Beta Rays hizi hazipenyi kwenye vitu kama Mbao ila zinapenya kwenye Karatasi.....wakati X rays zinapenya kwenye Karatasi na mbao...pia Gama rays zenyewe zinapenya kwenye Karatasi na mbao ila kuna sehemu hazipenyi kama kwenye lead na baadhi ya vitu kama Tofari kubwa la Nch 9

Kuhusu hizi aina za Radiation ni Story ndefu sana ilankifupi ni hivyo.......Na NUCLEAR MEDICINE inatumia GAMMA RAYS wakati CT SCAN NA PLAIN X RAYS zinatumia X-RAYS

Tazama picha hii kuelewa nguvu za hii mionzi uliyo taja wewe
radiation-penetration.jpg

Karibu kama unaswali jingine hasa katika Tiba n vipimo hizi za mionzi
 
Tazama picha hii kuelewa nguvu za hii mionzi uliyo taja wewe View attachment 506303

Karibu kama unaswali jingine hasa katika Tiba n vipimo hizi za mionzi
Ahsante ndugu, i like you...

Sasa nina swali la mwisho labda, zile scanner bandarini au airport zinatumia mionzi gani ambayo hupita hata kwenye chuma(contena)
Then unaposema mionzi ina madhara kidogo yaani kama dozi yake ni ndogo...je dozi inapokuwa kubwa maana yake ni nini? nasema hivyo nikimaanisha kuwa kama mimi siumwi je naweza kutumia hiyo mionzi kujichunguza just for funny!!!

Nataka kufahamu pia yale matibabu ya mionzi kwa cancer inatumia mionzi gani...nasikia pia ina maumivu sijui kwa nini
 
Hapo kwa Bandarini au airport siwezi kuongelea sana kwa sababu SIJUI ila kwa kifupi kwa ninavo jua mimi kuna aina 2 za bandarini au airport scanners

Na aina 2 hizi zote za scanners ni millimeter radio-wave na backscatter scanner,Millimeter radio-wave scanner zinatumia millimeter radio waves sawa na ile inayotolewa na simu nahisi na haitumii x-rays.Ila backscatter scanner,inatumia low intensity x-rays zenye nguvu kidogo!! Sina uhakika kama kweli inapenya au laah....NISIJE NIKAKUDANGANYA

Kuhusu wanao tibiwa kwa mionzi wale wa cancer ni kuwa wanaweza wakatumia moja ya aina ya mionzi hiyo hapo juu kuua Cancer kinacho tokea nikuwa wao wanatumia High energ Waves na dozi wanayo pewa......sasa hio mionzi inaweza ikatumika peke ake au pamoja na Chemotherapy au Surgery......

Pia kuna dawa mtu anaweza kupewa ili kufanya zile cells za kwenye cancer ziwe more sensitive kwenye Radiations......Mfano mtu wanatumia x ray kutibu sehemu yenye cancer lakini hyo sehemu haipo sensitive kwenye radiation wanacho fanya wanampa dawa kufanya hiyo sehemu iwe more sensitive to radiations.....Na pia mtu anaweza kutumia aiza hata zaidi ya mbili za mionzi kutibu the same cancer sasa hapo nadhani utakuwa unaona wapi mayumivu yanatoka!

Kwa upande wa Madhara iwe Dose kubwa iwe dozi ndogo madhara ni yale yale lakini mm nilisema Faida za hizi tiba ni kubwa kuliko madhara yake.....Sasa kuhusu madhara lbda uniruhusu naweza nikaelezea kwa ufupi

Madhara ya Mionzi Yanategemea Vitu vitatu

1.Kiasi cha mionzi anacho pewa

2.muda unao tumika kumpa hiyo dozi ya mionzi

3.Na sehemu katika mwili ambayo anapewa
 
Hapo kwa Bandarini au airport siwezi kuongelea sana kwa sababu SIJUI ila kwa kifupi kwa ninavo jua mimi kuna aina 2 za bandarini au airport scanners

Na aina 2 hizi zote za scanners ni millimeter radio-wave na backscatter scanner,Millimeter radio-wave scanner zinatumia millimeter radio waves sawa na ile inayotolewa na simu nahisi na haitumii x-rays.Ila backscatter scanner,inatumia low intensity x-rays zenye nguvu kidogo!! Sina uhakika kama kweli inapenya au laah....NISIJE NIKAKUDANGANYA

Kuhusu wanao tibiwa kwa mionzi wale wa cancer ni kuwa wanaweza wakatumia moja ya aina ya mionzi hiyo hapo juu kuua Cancer kinacho tokea nikuwa wao wanatumia High energ Waves na dozi wanayo pewa......sasa hio mionzi inaweza ikatumika peke ake au pamoja na Chemotherapy au Surgery......

Pia kuna dawa mtu anaweza kupewa ili kufanya zile cells za kwenye cancer ziwe more sensitive kwenye Radiations......Mfano mtu wanatumia x ray kutibu sehemu yenye cancer lakini hyo sehemu haipo sensitive kwenye radiation wanacho fanya wanampa dawa kufanya hiyo sehemu iwe more sensitive to radiations.....Na pia mtu anaweza kutumia aiza hata zaidi ya mbili za mionzi kutibu the same cancer sasa hapo nadhani utakuwa unaona wapi mayumivu yanatoka!

Kwa upande wa Madhara iwe Dose kubwa iwe dozi ndogo madhara ni yale yale lakini mm nilisema Faida za hizi tiba ni kubwa kuliko madhara yake.....Sasa kuhusu madhara lbda uniruhusu naweza nikaelezea kwa ufupi
Nashukuru kwa kidogo ulichonipa japo nataka kujua in depth kuhusu mionzi nawe sidhani kama unauwezo wa kunijibu in depth, hata hivyo nakushukuru
 
Ni kweli mkuu its very interesting kwenye hizi mambo....Mimi nitashindwa kukupa Kiundani sana kwa sababu Mionzi ina Vitu vingi sana wataalamu wanakwambia hata hili jua Pia.....Sasa huko duu

Ila kwa hzo Modalities hapo juu naweza semea
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom