Nianze na consultant!!
Katika ujenzi kuna watu watatu, yaani consultant, contractor na (clientemployer/initiator)!!
Nimeshakuelezea kuhusu contractor,
Tunaposema consultant kwa lugha rahisi tunamaanisha engineer!!! huyu anakua na jukumu la ku design structure na kuandaa michoro (engineering drawings) kulinga na mahitaji ya mteja yaani client au employer!!! injinia pia anaanda Bill of quantity (BOQ) kwaajili ya gharama elekezi za mradi au kujenga!!! BOQ inatumika kama mwongozo wa kumpata contractor kama client ataamua kumu-engage contractor!
Baada ya kumpata contractor au mjenzi injinia anakua na jukumu la kukagua kazi, kukagua material yanayoletwa site na zaidi ya yote injinia ndiye anaye andaa bill ya malipo ya contractor, na contractor analipwa tu baada ya injinia kuridhika na kazi iliyofanywa otherwise hamna malipo yatayofanywa!!! kikawaida injinia ni adui namba moja wa contractor (its a joke though)!! na injinia akilegea basi jua contractor kama sio mwaminifu basi lazima achakachue hasa kwenye nondo na cement (ratios)!
Ufahamu pia, client anamchagua injinia, then injinia anashiriki katika kumpata client ikiwa ni pamoja na kuandaa tender!!!
Tukija kwa msanifu majengo...
Huyu anajulikana kama architect! huyu kazi yake ni kuandaa michoro ya majengo, muonekano wa majengo, alignment za jengo and the alike!!! tofauti ya huyu na injinia ni kwamba injinia anafanya "engineering design na structural analysis"!! mfano ku specify nondo ya millimiter ngapi ikae wapi, ku design columns, beams, foundation na slabs!!! architects kikawaida hawafanyi haya!!!
Sasa baada ya msanifu majengo kuandaa michoro, michoro yake inapelekwa kwa injinia ambapo injinia ataichukua na kufanya engineering design kama nilivyo elezea hapo juu!!
Katika industry ya ujenzi msanifu majengo ndiye anachukua pay kubwa tofauti na injinia anayechukua 8-14% ya gharama za mradi!!! na architect pia anafanya inspections katika site kuhakikisha mambo yanaenda kama alivyo design!!!
Hawa wote wanafanya kazi kwa ukaribu, na kama mmoja akiwa lelemama basi ndio unatasikia jengo limeanguka!!!
Naimani mkifika chuoni hasa mwaka wa 3 au 4 mtafundishwa zaidi wala usihofu!
Karibu kama utakua na swali
Cc
mjuniour