Nitazibaje pengo la marehemu mchumba wangu?

Daltonae

Member
Jun 18, 2014
26
5
Ndugu zangu.Nasikitika kwamba nilimpoteza mchumba wangu mwaka jana katika ajali ya gari,

Niliumia sana,nilifadhaika sana,nilihisi watu wote kwangu ni wabaya,

lakini cha kusikitisha ni kwamba nimejaliwa kuwa na mahitaji yote ya kibinadamu lakini tangu nianze kutafuta mchumba january mpaka leo sijapata wa mwenye vigezo hata nusu kama wa awali,kwakweli ni swala ambalo limekuwa gumu kwangu,

Naombeni ushauri wandugu.
 
Pole sana mkuu....... Mioyo inauma na kusikitika sana pale unapokosekana uwepo wa wapendwa wetu... Usiwe na haraka ya kutafuta mchumba kaa tuliza akili. Usje ukapata wanawake wa kiswahili au wa watanzania hapo utakuja kutonesha kidonda cha pengo..
Ni vigum sana kuziba pengo
 
Asante sana 75 mm ila ungenipa extra mikakati ya kuweza kufanikisha hili swala.
 
pole mwaya

Mke na Mume mwema hutoka kwa Mungu hivyo kuwa mtu wa maombi utampata aliyewako

vilevile usipende kulinganisha watu , wanadamu wameumbwa kwa utoffauti sana huwezi kumpata yule atakayefikia yule mchumba wako wa awali itakuwa ngumu sana vinginevyo utavamia na viwewe bure kuwa mtu wa rohoni utampata tu
 
Pole sana Mkuu.

Nadhani KAMWE HUWEZI KUPATA MTU KAMA HUYO uliompoteza kwa maana watu tupo tofauti sana na kila mtu ana uzuri na upungufu wake.

Nachokushauri... Fungua moyo wako na ukubali uliempoteza hawezi kurudi, Pili ukubali kumpenda ambaye utaona ANAKUFAA bila kumlinganisha na yule wa zamani. kwa kufanya hivyo utaweza kumuona huyu kwa utofauti wake na kwa upekee wake. Ila ukitafuta mchumba COMPATIBLE, Nasikitika kukuambia hayupo huyo. ila Anayemzidi kwa kila kitu WAPO wengi na wanaomkaribia kwa kila kitu pia wapo wengi sana. Wewe tu UAMUE KUFUNGUA MACHO UONE.

Pole kaka maana kusema uhalisia saa nyingine inaleta maumivu.
Ndugu zangu.Nasikitika kwamba nilimpoteza mchumba wangu mwaka jana katika ajali ya gari,niliumia sana,nilifadhaika sana,nilihisi watu wote kwangu ni wabaya,lakini cha kusikitisha ni kwamba nimejaliwa kuwa na mahitaji yote ya kibinadamu lakini tangu nianze kutafuta mchumba january mpaka leo sijapata wa mwenye vigezo hata nusu kama wa awali,kwakweli ni swala ambalo limekuwa gumu kwangu,naombeni ushauri wandugu.
 
Mkuu tunapokuwa kwenye mambo mbalimbali kama sherehe,safari,masomoni,maofisini makanisani au misikitini automatically huko unaweza pata mchumba sio wa kutafutwa kwa kujitangaza.
GIDE MK,sidhani kama unaweza kupata kitu bila kukitafuta.
 
Asante kwa ushauri lady furahia ila sidhani kama mchumba anaweza kutokea bila kumtafuta.hata usalipo ni lazima umtafute.
 
Pole mpendwa kwa pigo ulolipata…usilinganishe watu kwani wanaadamu hotofautiana,huwezi kumrejesha mpenzio wa awali kwa kuwa na mtu anaelendana nae.Ni muhimu utambue unahitaji mtu mwenye vigezo vipi kisha uanze kumsaka lkn kumbuka kutafuta mwenzi ni kama kucheza kamari unaweza ushinde au ushindwe ila usivunjike moyo kwani ur better half is out there somewhere….
 
Leomimi najua watu wanatofautiana kidogo ila sio kigezo cha mimi kuchukua chochote.
 
Nawaza hapa...kwamba huyu Marehemu mchumba wako seem mlipendana sana...na kwamba ni chaguo lako...na kwa kuwa mafundisho ya Padri Marunda yanatuambia kuwa mke/mume mwema atoka kwa bwana...na kwa fact kwamba aliyekwisha kwenda kwa bwana harudi..ni kwanini nawe usisubiri saa ya bwana ili ukamfuate marehemu mchumba wako? Ni wazo tu...
 
Pole kakangu Mungu aendelee kukufariji lakini epuka kufanya ulinganisho tumeumbwa tofauti!
 
Pole sana ndugu, huwezi kupata mmbadala wa uliyempoteza... omba Mungu upate mwingine atakaye kufaa sio atakaye ziba pengo
 
Utampata , hata mimi nilimpoteza mke wangu lkn sasa ninamke mwingine and life goes on
 
pole sana usiwe na haraka ya kutafuta mbadala tulia jipe muda atakuja mwenyewe kwa muda muafaka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom