Nitawezaje kujifunza jinsi ya kutengeneza simu ?

Nitawezaje kujifunza jinsi ya kutengeneza simu ?

Chuck j

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2011
Posts
2,366
Reaction score
836
Wadau napenda kujifunza kutengeneza simu,,,,hasa software,,,,,,ku unlock na ku flashing ,,,.mwenye ujuzi plz ......
 
Hapa utakesha....
Mtafte m2 ukae nae uone anachafanya....hapo utafungua office yako
 
Wadau napenda kujifunza kutengeneza simu,,,,hasa software,,,,,,ku unlock na ku flashing ,,,.mwenye ujuzi plz ......

Mkuu mbona unaomba msaada kwa maneno machache hivyo utadhani unaomba maji ya kunywa?

Anyway, wapo wengi wanao hitaji kuJIfunza kama wewe unavyohitaji ila wamekosa pakuanzia kutokana na mazingira ya upatikanaji wa elimu hii ya mswala ya simu, mara nyingi watu wamekuwa wakijifunza kupitia kwa watu wengine ambao wemeshakuwa mafundi ni vyema huu muda ungeutumia kutafuta watu wanaojihusisha na huduma za kuflash huko maeneo ya kwenu, kutokana na uchache wa maelezo yako hayakutambulishi unakotokea hili ndiyo litakuwa jambo la msingi kwako.

Kwa ushauri tu endapo utamua kwenda kujifunza kuflash ni vyema zaidi ukatafuta fundi anaejihusisha na hardware na software upande wa simu, hii itakupa wigo mpana wakuweza kuijua simu vyema, mara nyingi wanoa jifunza software tu wamekuwa wakipata kizungumkuti, kuna wakati matatizo mengine ya hardaware hufanana naya-software, hapa unakuta simu ni yakuifanyia hardware fundi anakomaa kuflash mwisho wa siku anapoteza muda na simu inaishia kufa hivyo ni bora kama ukijifunza hardware na sofware, hata kwa mafundi computer wanakutana sana na changamoto hii.
 
Back
Top Bottom