Nitawezaje kuishi chuo bila mkopo, naombeni ushauri

Nitawezaje kuishi chuo bila mkopo, naombeni ushauri

Dah! mi mwenyewe nko mwaka wa pili nshasota saaaaana mpaka sasa ila nshazoea kwan wazazi wanajiita idi kidzaini japo ni wakulima.
so komaa broo utapasua tu kwani miaka inakimbia kama husn bolt.
 
Piga msuli.. we mtoto wa kiume ,mkopo sometime hupotezaga concentration ya mtu katika masomo.
 
Sina mkopo na life la chuo changu ( UDOM) kina ni favour mno chakula kwa siku nzima 3500 au 4000 ..nakomaa na Kuwa makin na matumiz ya pesa na Mzazi , ndugu na jamaa wanasaidia saidia hivyo hivyo
 
Pole sana ndugu yangu nimeona unatoka kagera nyumbani ,kikubwa nikujitambua.
 
Bila mkopo inawezekana tu iwapo una support nzur kutoka kwa wazazi, wafadhili au jamaa wengine. Ila watu hao wasipokua waelewa ujue utapata taabu kweli huko chuo cz ukimwomba pesa halafu akahis kama si ya lazima au vyovyote vile basi lazima utateseka tu chuo.

Fight upate mkopo ndo ukasome vinginevyo mm nilikua nna mkopo ila maisha kipind flan yalinibana sn pale Jordan Univ. College nikataka niche chuo kisa 20000 tu ya msosi cz boom lilichelewa na ndg kila niliemuomba anadai hana. Yale maisha sitaki kabisa kuyaishi tena . pole sn brother ila mkopo ni mzuri sn hasa kwa ss wanyonge.
 
D
Kaza buti mdau, mi nimesoma bila mkopo UDSM waka 2011-2014, nimemaliza, mama alikuwa anauza maandazi na baba alishaendaga kula mchanga tangu nilipokuwa form four.

Ushauri kaa sana na wana, mimi nilikuwa napigwa support na washkaji had nilipopata demu wa kizungu mwaka wa tatu nikawa nimesahau shida.

Ila mwaka wa kwanza na wa pili nilienda kwa mfanyabiashara maarufu akanilipia ada ya miaka miwili. Mungu amjalie ni Mzee anaitwa Zakaria pale kitumbini. kama vipi npm i have his number though kumuona ni kama unataka kumuona Bakhresa, You know what it takes... foleni sana.

Ila wana wamenipa support sana, I appreciate my friends at Univ of DSM.
Dah ati father ashaendaga kula mchanga aisee
 
Back
Top Bottom