Nitasema Kweli, Fitina Kwangu Mwiko!

Wateule

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
390
368
Kuna vitu viwili vya kuzingatia hapa, navyo ni (1) matendo ya mtu na (2) mtu. Matendo ya mtu yanapokuwa machafu, ya kinafiki, na ya dhulma; watu kumchukia au kumpinga mtu kutokana na matendo hayo. Lakini, mtu huyohuyo akigeuka kwa sababu moja au nyingine na kufanya au kuwa katika upande wa matendo yasiyo ya kinafiki na ya kupigania haki; watu humpenda ghafla kwa matendo hayo na kumuunga mkono.

Hivyo basi, kwa mfano, sio ajabu leo hii watu wengi kumuona Nape mtu mzuri (pamoja na kwamba matendo yake machafu ya huko nyuma tunayajua) kwa sababu aliacha unafiki na kuwa jasiri wa kutaka kusimamia haki. Lakini, kwa bahati mbaya watu wenye matendo machafu wamemuwai kabla hajamaliza harakati zake hizo. Kama Nape ataendelea na msimamo ule aliounyesha kwenye suala la Clouds na Bashite, basi ataendelea kujizolea wafuasi kwasababu watu huvutiwa na wa wasimamia haki. Ukiona watu wanabeza na kutowaunga mkono wapigania haki na ukweli, basi ujue wengi wa watu hao ni akili finyu zinazodanganyika kirahisi na wale waendeleza dhulma au watu hao wana maslahi ya moja kwa moja (direct) au ya pembeni (indirect) na waendeleza dhulma.

Kwa kumalizia, na kutokana na maelezo yangu hapo juu, sio ajabu kabisa kuona watu (wakiwemo watanzania mnao waita "manyumbu) leo hawamuungi mtu huyu mkono na kesho mtu huyo huyo wakamuunga mkono. Kwasababu, hii inategemeana zaidi na matendo ya mtu huyo katika wakati husika.
 
unajua tatizo kubwa LA watanzania ni woga na njaa ndo maana tunapelekeshwa hata na MTU mwenye zero yaani sifuri kwenye maarifa ya kufikiri. namalizia kwa kusema " FEAR OF LOST CREATE A WEAK MIND"
 
Back
Top Bottom