Nitapataje Mtaji Wa Mil.1 Kuanza Biashara Ya Nafaka Baada Ya Chuo

joseph mzuma

Member
Dec 31, 2015
58
50
Habari Wanajukwaa

Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuo kikuu cha Dodoma(UDOM)

Natarajia kuhitimu masomo mwezi wa saba (July) mwaka huu.(2016).

Profesheno yangu ni Ualimu, tena ni Mwalimu wa Sayansi masomo ya Chemia Na Biolojia

Ndoto yangu ni kuwa Mfanyabiashara, biashara inayohusika na NAFAKA.

Naipenda Biashara hii kwani ndiyo ilikuwa inamwezesha mama enzi za Uhai wake kunipatia mahitaji ya shule hadi nikapata kufika hapa nilipofika leo na zaidi ni biashara ambayo WATEJA wake ni watu wa tabaka zote siyo masikini wala tajiri kila mtu anahitaji Nishati kutokana na kula Nafaka ivo ni biashara yenye wigo mpana na biashara ya kudumu

Baada ya Masomo, Mipango yangu ni kuanza kuiishi ndoto yangu kwa kujishughulisha na kununua Mpunga kwa wakulima na kuukoboa kisha kuuza mchele kwa kulingana na hali ya mzunguko wa biashara utakao kuwepo kwa wakati huo au ukizingatia mwezi wa 7 kitakuwa kipindi cha mavuno ivo mpunga utakuwa wa bei nafuu naweza kununua na kuuweka stock nikisubiri upande bei.

Changamoto yangu kubwa ni sehemu ya kuanzia yaani sina mtaji Naomba Mwenye Uwezo au Uelewa wa namna yoyote ile ya kunisaidia nipate angalau milioni 1 za kuanzia biashara hii. Niko tayari kwa masharti yoyote yasiyo kandamizi katika kukua na kuendelea kwa Ndoto yangu
Natumai mtaendelea kutumia Busara katika kuchangia hili suala langu
Mungu awatangulie.................

mNapatikana kwa mawasiliano

+225 783 939 474
 
Maliza chuo, Pata kazi then kupitia hiyo kazi anza kuweka some amount of money kwa ajili ya kuanza hiyo biashara.Jitathimini after one year then kama biashara imekuwa vizuri, unaweza kuomba mkopo bank zenye masharti nafuu ili kukuza biashara yako.
 
as

Ahsante mkuu, Mungu akubariki kwa ushauri mzuri
 
Kwa sasa umebakiza maboom mawili na field kwa nini usitumie vizuri hilo boom lako??
Ahsante sana Mkuu kwa ushauri wako nimeupata, Kwa UDOM mwaka wa tatu hatuna field, maboom mawili nashukuru nitajibana lakini nimejibana vya kutosha toka first year nikaona niulete huu uzi hapa baada kuona safari niliyonayo huko mbele. Niseme tena nashukuru kwa mchango wako pia
 
Million moja siyo nyingi ku raise ukiwa na malengo. Get a job first...hata kama ni kubeba zege. Then save kidogo kidogo wakati pia unaweka ramani zako sawa. Mwaka huu unaweza kuchelewa, then aim kwa msimu ujao.
 
Save ilo boom achana na habari ya tamaa kununua simu za bei mbaya,nunua tecno y3+ iwe mkataba,
Acha kwenda club, acha kuhonga,acha kuweka vocha bila sababu, usipende kula kula hovyo hovyo, vaa mtumba! In short kuwa na attitude ya kibahili* Utafanikiwa sana mpk ukimaliza hutokosa mil 1 na nusu
 
mbinu nzuri sana hii ya kuwa bahili na mimi na amini katika kujibahilia bahilia kuna kuaga na impact kubwa sana kama kweli mtuu umeamulia kufanya lengo lako. na ukiwa makini na ubahili utafanikiwa . mbinu ya tajiri kufika alipo fika ni ubahili tu. hakuna kingine!
 
Million moja siyo nyingi ku raise ukiwa na malengo. Get a job first...hata kama ni kubeba zege. Then save kidogo kidogo wakati pia unaweka ramani zako sawa. Mwaka huu unaweza kuchelewa, then aim kwa msimu ujao.
Ahsante mkuu, Nashukuru kwa stragies ulizonifunulia na ushauri mzuri mi nashukuru ntazifanyia kazi
 
Save ilo boom achana na habari ya tamaa kununua simu za bei mbaya,nunua tecno y3+ iwe mkataba,
Acha kwenda club, acha kuhonga,acha kuweka vocha bila sababu, usipende kula kula hovyo hovyo, vaa mtumba! In short kuwa na attitude ya kibahili* Utafanikiwa sana mpk ukimaliza hutokosa mil 1 na nusu
Mkuu extrovert Nashukuru kuniongezea mbinu za kufika mbali kimaisha, Ni miongoni mwa vitu vinavyotushinda vijana nimekua nikiviamini haviwezi kunifikisha nakotaka kufika na Namshukuru Mungu niko tofauti nakushukuru sana kunisisitizia Mungu akubariki nitajitahidi kuyaishi
 
Kijana hongera sana kwa mawazo mazuri ulijaliwa na MUUMBA wetu.Bila ya kukuficha mafanikio yote hutokana na nia uliyonayo.Ninacho kukuambia usifikirie lazima upate hiyo milioni moja ndio uanze biashara ya nafaka.hata ukiwa pungufu wewe anza tu kijana.
 
Back
Top Bottom