Kiongozi wa mapinduzi wa jamhuri ya africa ya kati, jamaa ana mambo kavunja bunge na taasisi zote za serikali na kasema atakuwa rais kwa miaka mitatu huku akiiweka katiba kando. Nilichojifunza kwenye mgogoro huu wa CAR , ni kuwa wafaransa walishamchoka francoise bozize walitaka aondoke so ilikuwa suala la muda.
Kama kuna mkoloni wa zamani ambaye anasimamia maslahi yake kwenye koloni zake za zamani ni ufaransa, hana mchezo , kafanya tricky game CAR lakini pia kaamua kuingia Mali ndani ya muda mfupi. Waingereza nao wakiamua wanaweza kufanya lolote hapa kwetu hasa baada ya huu urafiki wetu na wachina.