Nitampataje msichana huyu???

ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
4,210
555
Wana jamvi habarini, ni hivi nimemtongoza msichana ambaye kwa namna moja ama nyingine ambaye nimempenda kiukweli, tatizo ni kwamba ameathirika kisaikolojia kwa kuwachukia wanaume kwa sababu siku za nyumwa alitendwa na boy friend wake, hata hivyo mpaka sasa mambo bado hajaeleweka, yeye anadai kwamba kila akikumbuka maumivu aliyoyapata anakosa amani, na anasema bado hajawa tayari. Ndugu wana jamvi nifanyeje au mambo gani niyafanye kwa mrembo huyo ili niweze kuwa naye? Karibuni kwa ushauri wenu maana nimetokea kumpenda sana huyu binti!
 
Kama mwenyewe anasema bado hayuko tayari basi heshimu hilo na mpe nafasi yake kwa sasa hadi hapo labda atakapokuwa tayari (kama anachosema ni kweli na si kibuti cha kidiplomasia).
 
Muongo huyo usikute yeye ndo alimbwaga huyo mshikaj wake wa mwanzo.mtafutie mazingira tu ukammege
 
mvumilie huku ukionesha upendo wa dhati,itafikia mahali ata kukubali tu,usimlaumu kutendwa kubaya huwezi jua alifanyiwa nini,just cool down na usikate tamaa na wala usiwe mtu wa kumlazimisha just msikilize matakwa yake kwanza itafika mahali mtaelewana tu!
 
Wana jamvi habarini, ni hivi nimemtongoza msichana ambaye kwa namna moja ama nyingine ambaye nimempenda kiukweli, tatizo ni kwamba ameathirika kisaikolojia kwa kuwachukia wanaume kwa sababu siku za nyumwa alitendwa na boy friend wake, hata hivyo mpaka sasa mambo bado hajaeleweka, yeye anadai kwamba kila akikumbuka maumivu aliyoyapata anakosa amani, na anasema bado hajawa tayari. Ndugu wana jamvi nifanyeje au mambo gani niyafanye kwa mrembo huyo ili niweze kuwa naye? Karibuni kwa ushauri wenu maana nimetokea kumpenda sana huyu binti!

simple sana hiyo. mimi hao huwa nawapenda sana coz nami huwa najifanya nimeathirika kisaikolojia, fanya hivi
1. Usitangulize kutaka kummega mapemaaaa, uwe na subira sanaaaaa taratibu kama hautaki vile atakuja mwenyewe...Jitahidi kuwa wazi kwake na muonyeshe kumjali, akiwa na shida yoyote hiyo onyesha ushirikiano wa kutosha, akipiga simu wahi kupokea, hata wewe jitahidi kwa mawasiliano japo vitext 10 kwa siku si mbaya, ukiamka,before tea, kama anafanya kazi around sa 5 -6 hivi mpe pole ya kazi, sa 7 hivi mstue luch, sa kumi hivi mpe pole ya kazi.. etc
2. acha kumuulizia ulizia habari za huyo boyfrendwake (x), licha ya kwamba inawezekana yeye (she) ndiye alimtosa jamaa kwa tamaa zake take care
3. Jitahidi kuongea naye kwa ukaribu na utaratibu, usijanye unajua sana uwe unamwacha yeye anaongea, kama kunajambo anataka kufanya lipime kama ni jema mpe moyo sana alifanye
4. kama uko njema sana jitahidi uwe unamualika sehemu tulivu za wazi kwa soft drinks etc, halafu mshirikishe sana mambo yako kama kuna jambo unataka kufanya jifanye kama unamuomba ushauri hivi yeye, yaani kwa ishu yoyote ambayo unaona si mbaya akiijua wewe mshirikishe, ataona unamjali sana na unamuona yeye kama ni mtu muhimu sana na ni nguzo muhimu sana kwako, kumbe unamalengo yako tu.

ukitaka kula sharti uliwe.. fanya hayo kwanza then after 3 months utanipa majibu, lazima ataanza kukutext yeye na kupenda kuwa nawe, na ataanza kufunguka kwako kwa mambo mengi, but usiwe na haraka ya kupiga dushe, mengine ntakupa siku nyingine mkuu.

pamoja
 
mvumilie huku ukionesha upendo wa dhati,itafikia mahali ata kukubali tu,usimlaumu kutendwa kubaya huwezi jua alifanyiwa nini,just cool down na usikate tamaa na wala usiwe mtu wa kumlazimisha just msikilize matakwa yake kwanza itafika mahali mtaelewana tu!
nakushukuru mkuu.,.nitajitaidi...
 
nitajitaidi mkuu, lakini nipe hata baadhi ya mambo yatakayomfanya asahau namna alivyotendwa...

mjenge kisaikolojia akuamini then taratiiibu ataanza kufoli in love na wewe.outing,zawadi za vitu anavyopenda,suprises,onyesha kuwa upo tayari hata kuwatembelea ndugu na jamaa zake,pia mtambulishe kwa ndg zako(do all that as a friend,means onyesha kuwa umekubali kumpa muda but akubali kuwa friends na wewe) etc.show her that ur different sio wa kulialia na mimacho ya tamaa ya ngono umeitoa utadhani umekutana na kigoli yupo uchi barabarani!!!
 
tafuta ka-tempo pembeni huku ukiwa unaendelea kumsaidia kisaikolojia huyo mwingine.
 
mh aisee been there done tht, inawezekana kweli kaumizwa ila pia inaweza ikawa kaswaga au hajakukubali kivile....
 
me nishamjua msichana unayemuongelea si anaitwa amina madina! kama ndo huyo huwezi kumpata mana alitendwa vibaya sana...
 
Back
Top Bottom