Nitampata wapi mwingine?

Nitampata wapi mwingine?

Quetzal

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
6,345
Reaction score
10,842
Kumekuwa na Hali ya sintofahamu inayowakumba wadada au wanawake wengi, wanavumilia vipigo, manyanyaso matusi, kebehi nk. Hapa naongea na wadada ambao Bado hawajaingia kwenye ndoa sijui ambao wameolewa.

Mahusiano mabovu mtu hakujali Wala haoneshi kukuhitaji lakini wewe unang'ang'ania eti NITAMPATA WAPI mwingine. Mahusiano Kila siku vipigo unahonga mwanaume unamjali na Kila kitu unamfanyia lakini yeye haoneshi kukuhitaji.

Mtu hajali hisia zako, umeshalazimisha, umeshahonga umeshamzalia lakini hakutaki..walk away it's called SELF RESPECT.

Jipende jithamini na jijali. Jipende Sana kiasi kwamba ujue limit zako kuwa Siwezi vumilia hiki na hiki katika haya mahusiano, jipende na jithamini kiasi kwamba ujue unastahili kilichobora.

Using'ang'anie mahusiano ambayo hayana Tija eti NITAPATA WAPI MWINGINE. Utampata huyo mwingine kwani yupo na atakujali na kukuthamini na utakuweza kufurahia mahusiano..Do not settle

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanawake wengine wanakumbwa na hiyo karma ikizingatia unakuta walishawahi kuwakataa wanaume waliowapenda kwa dhati. Sasa hapo akiangalia hana namna kwa hiyo ameangukia kwenye penzi la mateso. Na anajikuta akiwa mpweke anaumia zaidi kwa hiyo bora akae hapo anapopokea kipigo na dharau.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom