Nitakukumbuka sana baba yangu

nusuhela

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
6,632
Reaction score
8,452
Nimeanzisha uzi huu ili kukuenzi baba yangu mzazi niliyekuzika jumapili ya tar 29/7/2018.
Ulifariki usiku wa kuamkia ijumaa tar 27/7/2018. Ulifikwa na umauti ukiwa unakimbizwa hospitali baada hali yako kuwa mbaya ukiwa unatokea mkoani Mwanza ambako ulienda kutoa mahali ya mdogo wetu wa mwisho ambaye alikua anaoa.
Ninaamini uzi huu utaishi milele.
 
Ni miaka 20 imepita tangu anitoke mamaangu,ni miezi 7 imepita tangu nizike baba yangu.
Pumzikeni kwa amani wazazi wetu,kazi yenu mliitenda vyema. Mungu awafariji wote mlio ondokewa na wazazi wenu
[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Ni mwaka mmoja tangu anitoke Baba angu mpendwa..nakumbuka Mara ya mwisho kuongea nae aliniambia mwanangu kesho narudi nyumbani tutasherekea sikukuu wote.. Siku iliyofuata tunaletewa taarifa amefariki kwa ajali ya pikipiki...pumzika kwa Amani Mzee wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…