Nitajuaje idadi ya samaki wanaopaswa Kuja kuwekwa kwenye bwawa:

Kigoma Independent

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
3,519
2,047
Kwanza kabisa uwekaji wa samaki kwenye bwawa huwa Ni kwa idadi maalumu kwa kawaida.
Kitaalamu,mita 1 ya mraba unaweza kupandikiza samaki kuanzia 3-5,6-10,11-15,16-30,kwamfano bwawa likiwa la mita za mraba 600×samaki 5=samaki 3000.Idadi hii ya samaki huwekwa kutokana na sababu zifuatazo ambazo husababisha kufanya maamuzi ya kuweka samaki kutoka 3-30 ambazoni:
✓upatikanaji wa maji ya kutosha na uhakika.Ambapo usaidia kutambua idadi ya samaki kutokana na kiasi Cha maji kilichopo katika bwawa.Kwamfano,bwawa lenye ukubw wa mita 2 kwa mita 3,ambalo jumla ya mita za mraba za eneo 6,mfugaji anataka kuweka samaki 500/1000.Ko kukiwa na maji ya kutosha kuta muwezesha mfugaji aweze kutambua ukubwa gani wa mraba wa bwawa wa kuweza kutumia kwa kulinganisha na kiasi Cha maji na pia samaki.
✓Uwezo wa uhakika wa kulisha samaki kwa kipindi chote cha ufugaji.Hii Ni kutokana na kutathimini kiasi ch chakula ambacho samaki wanaweza kukipata kwa kulinganisha na uwezo ulionao.Kwamfano,samaki 1000kipindi Cha ufugaji Cha miezi 6,samaki 1000 watakula kilo 90,Kama bei ya kilo 1 Ni shilingi 2000,jumla ya gharama Ni shilingi 180,000.
Na miongoni mwa faida zitokanazo na kufuata utaratibu Ni;
•samaki kukua haraka.
•maji kutochafuka kwa haraka bwawani.
•samaki kutodumaa/kutokufa.
•kuepuka magonjwa ya samaki.
Pia,miongoni mwa hasara zitokanazo na kutokufuata utaratibu Ni;
°samaki kuto kukua haraka.
°maji kuchafuka kwa haraka bwawani.
°samaki kudumaa/kufa.
°magonjwa ya samaki.
N.B:maji yakiwa madogo kwenye bwawa hakuna athari yeyote ambayo itatokea kwa samaki.
 
Option ya kufata ni kuonana na mtaalamu kaka akakushaur zaid...kwa mfano kwenye sq mita 6 huwez weka samaki 1000
 
Option ya kufata ni kuonana na mtaalamu kaka akakushaur zaid...kwa mfano kwenye sq mita 6 huwez weka samaki 1000
Mimi Ni miongoni mwao na inawezekana kwasababu ninmeshatoa masomo mengi zaidi ko unaweza ukani pm for more explanation
 
Hayo ma bwawa yanakuwa yameunganishwa na maji yanayoingia upande mmoja na kutokea mwingine ama yanakuwa yamejazwa tu kisha yanatuama hadi yabadilishwe tena?
 
Back
Top Bottom