Nitaitambuaje chaji ya Iphone ambayo ni orijinal?

Smiller

Senior Member
Joined
Feb 10, 2014
Posts
181
Reaction score
41
Msaada jamani maana kila chaji ninayo nunua haimalizi mwezi inakufa!! Wakunijuza tafadhali nawapi zinapatikana
 
Nenda mcity wana store yao, ukishindwa agiza online ambako zipo cheap.

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
Msaada jamani maana kila chaji ninayo nunua haimalizi mwezi inakufa!! Wakunijuza tafadhali nawapi zinapatikana
maranyingi charger original za iPhone huwa zinakuja in two pieces yaani (usb cable na wall adapter). original usb cable huwa ni mlaini ukilinganisha na fake usb. Ndani ya kichwa cha usb original, ukiangalia kupitia vishimo viwili utaona connectors zina rangi ya gold wakati kwenye feki kuna connectors za rangi ya silver. pia juu ya kichwa cha usb original kuna symbol iliyo na light grey color wakati kwenye feki ina dark grey color. lakini kikubwa zaidi cha kuzingatia ni ile wall charger kwasababu feki huwa hazipitishi moto unaotakiwa na unaweza kuua nguvu ya battery ndani ya muda mfupi. Original zinakuwa na power output ya 0.15A wakati feki zinakuwa na 0.1A kwenye label yake kwa chini. hicho ni kitu muhimu sana cha kuzingatia. Kanunue wall adapter yenye 0.15A na usb cable nzuri tatizo lako litakwisha..
'O' - Original
'C' - Copy(fake)



 
Last edited by a moderator:
nimejifunza kitu leo credit kwako mkuu iwe mwendelezo wa kujulishana na kufahamishana jinsi ya kutambua electronic devices original na fake.
 
update simu yako kwenda ios 7 watakupa warning kila ukichomeka charger feki
kwa situation ya mdau hapo juu naona kwenda ios 7 haitamsaidia kwasababu hata ios 6, 5, 4 ,3 etc zinaweza kudetect accessory ambayo sio compatible na simu. na pia sio iphone zote zinaweza kwenda ios 7. cha msingi hapo ni kuzitambua hizo original chargers
 
Mkuu nataka nikanunue iphone five juma tano .je niangalie nini na ni ili nijue kama ni feki au orignal msaada wako kwanza
 
Charger original ni ile inayokuja na simu....hizi zinazouzwa mitaani hata huko mlimani city sio original.
 
Mimi ndani ya mwezi nanunua chaja mbili. Zinakufa sanaa
 
Mimi ndani ya mwezi nanunua chaja mbili. Zinakufa sanaa

Ni charger inayokufa ama Lightning ChargeSync Cable?

Nachojua kinachosumbua kwenye simu za kuanzia iPhone 5 ni hiyo Lightning ChargeSync Cable ambazo zinakufa mara kwa mara, na ni tatizo kubwa na watumiaji wa iPhone 5 wanailalamikia sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ