Nitaishitaki CCM mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nitaishitaki CCM mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kurzweil, Jun 26, 2012.

 1. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 4,868
  Likes Received: 4,712
  Trophy Points: 280
  [h=6]Nitaishitaki CCM Mahakamani, Bado najadiliana na wakili wangu kuhusu hilo.

  Nia ninayo, Uwezo ninao, na Sababu ninazo.

  ... Baadhi ya mashitaka yatakayoainishwa ni:

  Kupigwa kibao nikiwa mtoto mdogo (1985) na kada wa CCM, pale nilipouliza swali la msingi baada ya kuiona karatasi ya kupigia kura hasa ukizingatia wakati ule hakukuwa na haja ya kujiandikisha kupiga kura, unaenda tu kituoni unachukua karatasi na kuijaza. Msingi wa swali langu ni hoja, nilimuuliza msimamizi wa kituo " hivi hakuna mgombea mwingine hapa ili tumchague?"

  Ile karatasi ilikuwa nyembamba na ndefu kidogo, halafu ilikuwa na sehemu mbili za picha, upande wa kulia ilikuwa picha ya baba aliyejaa mashavu, mwenye tabasamu na mvi moja moja kwa mbali,na chini yake kuna alama ya V au ndio. Upande wa kushoto kulikuwa na sehemu ya picha yenye kivuli (giza) na chini yake alama ya X. Hapo ndipo nikauliza swali langu la msingi na kupigwa, sasa basi kwanini nipigwe badala ya kujibiwa na kama ilivyo kawaida kwa watoto kuuliza maswali hata 200 ikibidi.

  Pili niliona watoto wakipiga kura kwa maelekezo kwamba"njoo jaza hapa"ulikuwa ni utani wa kweli.

  Sababu nyingine ni kubakwa : Uhuru wangu ulibakwa mwaka 1987, pale nilipolazimishwa kuimba nyimbo zenye hamasa ya chama cha mapinduzi bila idhini yangu. Shuleni mimi nilikuwa mtafsiri wa lugha ya kiingereza kwa wenzangu, M/kiti wa kamati ya "maadili lugha " ila kila siku asubuhi niliamriwa kuimbisha wenzangu nyimbo za CCM" Chama chetu cha mapinduzi chajenga nchi", Aaaah TANU na CCM vyajenga nchi, na nyinginezo nyingi, nilipokataa nilipewa adhabu mbaya sana, Kwanza mwalimu mkuu, (Mwl Daudi Minja soma hii)aliniingiza ofisini kwake, akanichapa viboko ambavyo havina idadi....

  Kulazimishwa kutoa Sh 5, kama mchango wa mafuta ya mwenge hata kama hakukuwa na mwenge, mwalimu wa uhamasishaji alikuwa kada wa CCM (Bibiana Tarimo)..jamani wote hawa wapo tena bado ni waalimu na wanaendelea kufundisha (Naomba nisizitaje shule wanazofundisha,na waliopandishwa vyeo kuwa waratibu wa elimu hadi nitakapo wasiliana na mwanasheria wangu).

  Jina langu kupewa mtu mwingine na akasoma kwa jina langu katika shule moja kule Arusha huku mimi nikisoma shule ya bei mbaya kwa kujishughulisha na kuombaomba mitaani hadi kufikia hatua ya kusaidiwa na kanisa (Naomba nisiitaje kwa sasa kutokana na taratibu za kesi kutokamilika) kwa kutumia majina yangu matatu..huyu niliwahi kutana naye nikamuuliza na kumdadisi akanieleza ukweli wote...huyu ni key person kwani atakuwa mmoja kati ya mashahidi. Baba yake ni kada wa CCM, hivyo naamini atatupa ushirikiano wa kutosha. Yote haya yalifanyika kwa kauli mbiu ya kuwaandaa vijana wa kakamavu wa CCM....tupewa mifano mingi ya jinsi Lord Powel, mwanzilishi wa Scout huko Uingereza!

  Hayo ni baadhi ya yale yatakayoainishwa na kujumuishwa katika hati ya mashitaka.

  Naomba mwongozo!!![/h]
   
 2. 1

  19don JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  wahi mahakamani mkuu ni haki yako kikatiba(hii iliyochakaa)
   
 3. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  hahahahaha....! kweli mkuu..! kila uchaguzi raisi anashinda kwa 99%.
   
 4. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 4,868
  Likes Received: 4,712
  Trophy Points: 280
  Nakaribisha mashitaka ya nyongeza
   
 5. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Mwanasheria wako anasemaje? sababu kazi kubwa ni kuprove kwamba CCM was a privy to all of your cases? timing nzuri ya kulodge hii case in 2015 kama kweli unataka watu washughulikiwe lakini kama unataka hizo kesi zako zichukue mkondo wa kisiasa naamini utakisababishia hiki chama matatizo makubwa sana.

  Ushauri wa msingi ni kuangalia namna gani watu wengi zaidi tutashiriki kufungua hiyo kesi sababu hata mimi ni muhanga.
   
 6. Davie S.M

  Davie S.M JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 720
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kwani Umri wa Kupiga Kura ulikuwa Miaka Mingapi....maana ulikuwa unasema ulikuwa mtoto....Hakika hii itakuwa kesi ya Mwaka.

  Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
   
 7. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  wapeleke magamba but be care with Nepi maana anatembea na Rushwa tayari tayari
   
 8. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Unaitwa nani? (majina matatu)
   
 9. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,904
  Likes Received: 2,322
  Trophy Points: 280
  Kuna jamaa anaitwa CHADEMA kazi hiyo hiyo inaelekea kumlemea.
  Miye nakutakia kila la heri, ila usijepata maumivu ya kichwa katika harakati zako.
   
 10. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  jf ndo mahakama,umesema unaongea na wakili wako,sasa jf umefata nini
   
 11. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Tangulia tutakukuta mahakaman
   
Loading...