Nitaisambaratisha CCM Kanda ya Pwani-Mabere Marando

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Makamu Mkiti wa Kanda ya Pwani wa Chadema Mabere Nyaucho Marando amesema kwamba ataisambaratisha CCM katika kanda hii.

Huku akishangiliwa kwa mayowe na wajumbe na viongozi wa kanda hii inayojumuisha Dar es Salaam na Pwani,Marando amesema yeye amesomea ushushushu na atatumia Taaluma yake hiyo kuhakikisha CCM itabaki historia katika kanda hii.

Marando amesema atafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha anadhibiti mbinu zote za CCM.Na atatembea kila kona ya kanda hii kuizika CCM.

Viongozi wengine wa Kanda hii ni Mkiti Professor Abdallah Safari na Katibu wa Kanda Halima Mdee.

Marando ameongeza kwamba anaongoza kanda kubwa yenye watu wengi ambao idadi yao ni kama nchi ya Rwanda au Shelisheli.Hivyo ameahidi utumishi uliotukuka.
 
Bila shaka lazima isambaratike!
 
sijui kachora mkanda mashshu hawaachi kazi yao mpaka kufa
 
Ni kiapo kizuri, tunamtakia kila la kheri, tunamuahidi ushirikiano wa hali na mali katika kufanikisha mkakati huo wa ukombozi wa Taifa toka kwa mkoloni mweusi/kaburu ccm.
 
ameshindwa tangu zamani waliokuwa wanamshangilia hawajui kama bado anaitumikia tiss hadi kifo chake,aka pandikizi time wil tel on his peach
 
""amesomea ushushushu na atatumia Taaluma yake""

mbona hatujaona makucha ya taaluma Hiyo kwenye ile video....
 
sijui kachora mkanda mashshu hawaachi kazi yao mpaka kufa
Haswa ndicho alichosema! atatumia taaluma yake kikamilifu Kukisambaratisha Chama Cha Magamba katika kanda hii!
Safi mno
 
Makamu Mkiti wa Kanda ya Pwani wa Chadema Mabere Nyaucho Marando amesema kwamba ataisambaratisha CCM katika kanda hii.

Huku akishangiliwa kwa mayowe na wajumbe na viongozi wa kanda hii inayojumuisha Dar es Salaam na Pwani,Marando amesema yeye amesomea ushushushu na atatumia Taaluma yake hiyo kuhakikisha CCM itabaki historia katika kanda hii.

Marando amesema atafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha anadhibiti mbinu zote za CCM.Na atatembea kila kona ya kanda hii kuizika CCM.

Viongozi wengine wa Kanda hii ni Mkiti Professor Abdallah Safari na Katibu wa Kanda Halima Mdee.

Marando ameongeza kwamba anaongoza kanda kubwa yenye watu wengi ambao idadi yao ni kama nchi ya Rwanda au Shelisheli.Hivyo ameahidi utumishi uliotukuka.
Vipi hajaongelea maendeleo ya kanda hii zaidi ya kujiandaa kuidhibiti CCM? Kazi iPo.
 
Tangu alipoivuruga NCCR Mageuzi, sina imani tena na Marando.....
 
Back
Top Bottom