Nitagombea Urais wa Zanzibar 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nitagombea Urais wa Zanzibar 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msema hovyo, Jul 10, 2011.

 1. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #1
  Jul 10, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ndugu watanzania wenzangu, nimeona nijitokeze hadharani na kuiweka wazi nia yangu ya kugombea urais wa zanzibar kupitia CUF. Nimeshawishika kugombea urais wa zanzibar ili kutekeleza yafuatayo:
  1. Ni kuhakikisha tunapata Zanzibar huru inayojitegemea kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa na kijamii. Nitasimamia kuvunjika kwa muungano wa Tanzania na kujiunga mapema katika East African federation kama nchi huru.
  2. Kukuza shughuli za kiuchumi za Zanzibar ambazo ni dhahiri lakini hazijapewa kipaumbele kwa maendeleo ya wazanzibari. Na hizi ni pamoja na utalii, uvuvi, kilimo na biashara
  3. Kusimamia na kuboresha elimu ya wazanzibar, kwa kuongeza idadi ya wazanzibar wanaojiunga katika elimu dunia (ya shule ya msingi hadi chuo kikuu)
  5. Kujenga umoja na mshikamano wa wazanzibar kwa kuunganisha nguvu za pamoja kati ya Pemba na Unguja. Katiba ya Zanzibar mpya itahusu mgawanyo sawa wa madaraka kati ya wapemba na waunguja
  6. Nitajielekeza zaidi katika kuboresha maisha ya watu wa Pemba ambao kwa muda mrefu walisahauliwa sana kiuchumi, hasa katika nyanja za usafirishaji, afya na elimu.
  Nitawaletea mengine mengi kadri siku zinavyokwenda. Ninaomba munikosoe katika haya, ili hapo nitakapoliweka wazi jina langu kwenu, muwe tayari mnajua mimi ni mtu wa namna gani. Kwa sasa naomba mnijadili nikiwa under cover.
  Nawasilisha.
   
Loading...