hivi Kangi Lugola ni member wa humu jamvini? jamani mjulisheni jimbo linakwenda kwao.
Mgombea mtarajiwa - mbona kuna barabara safi kabisa kutoka Bunda hadi Kisorya na kwingineko na mh.Kangi ni mwekezaji mzuri/mkubwa katika masuala ya hiece toka Bunda town hadi huko kwenu na anatoza a competitive fare - wengine wanafanya shs.3,500 - 5,000 kwa kichwa yeye anafanya 1,500 nauli kwa kichwa.
Kwa ufupi, lawama nazipeleka kwa wabunge wote wa mkoa wa Mara, hawana mkakati wala solutions za matatizo ya wananchi wao, wote ni hovyo: kwa upande wa barabara mkoa hauna barabara ya lami hata moja ambayo imetokana na mkakati wa nchi ukilinganisha na mikoa mingine, hio barabara iliyopo ipo kwa sababu maalumu, kwa upande wa elimu ni jimbo la Musoma vijijini ndio lenye ahueni, ukija suala la uchumi haviendani kabisa na fursa za ziwa, ardhi, mbuga na madini vilivyopo, infact mkoa wa Mara haustahili kuwa na maendeleo iliyonayo sasa.
Kazi kwenu wah.watarajiwa ila mie pia nakuja - bado sijajua jimbo la kuchukua nasubiri kuoteshwa kwanza tutakutana mbele ya safari, hata kwa TLP ama ACT lazima Mara ikombolewe