Nitafikishaje huu ujumbe kwa DC Kisarawe

Nitafikishaje huu ujumbe kwa DC Kisarawe

wakurochi

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Posts
2,647
Reaction score
2,954
Mi mkulima Kisarawe vijijini. Mimi sio mzawa ila nimehamia huko muda sio mrefu kulima, Kijiji kinaitwa Yombo Lukinga.

Kumekuwa na tatizo la wafugaji ambao ni ndugu zetu wamang'ati kulisha mifugo yao kwenye maeneo ya makazi ya watu na hata mifugo yao kuingia na kuharibu mashamba yetu. Na pia mifugo yao kuchangia visima vya maji ya kunywa na sisi wakazi. Yaani ni sawa na kusema mtu anakaa na mifugo yake pale Jangwani (DSM) lakini anaamua kupeleka mifugo yake mpaka FIRE halafu pale anakata kulia anaenda na mifugo mpaka Msimbazi na mtaa wa Uhuru mpaka mnazi mmoja kila siku.

Hilo ndio Tatizo kubwa pale. Wananchi baada ya kulalamika sana, wafugaji wamehamisha mifugo yao ila wamebaki wafugaji watatu tu ambao inaonekana hata wakulima tupige kelele vipi hawsaondoki na hawasikii. Mbaya zaidi wanafungulia ndama wajichunge wenyewe na ndama wanavamia tu shamba lolote lenye chakula. Wafugaji mifugo ikishiba wao kwao ni furaha haijalishi wamekula wapi.

KWANINI NIMEAMUA KUWA WHISTLE BLOWER

Uongozi wote wa kijiji na Mwenyekiti wanawapeleka barua hawa wafugaji wahame, wafugaji wanapokea barua na kudharau tu na kuendelea na tabia ile ile. Mwenyekiti na Wenzake dana dana nyingi sana kwetu wakulima.

Pili, ukionekana uko mstari wa mbele kuwatoa wafugaji wana kisasi sana, unaweza kuchomewa banda lako na pia hawa viongozi utaonekana umewashitaki na hii itasababisha ukazi wako kuwa mgumu pale kijijini.

Hivyo naona njia sahihi ni kuwafikishia taarifa "anonymously" wahusika ili wazijchunguze na kuzifanyia kazi.

Wala sidhani kana kuna shida ya DC kwenda kule, mi nadhani akiamua kupiga simu tu kwa mtendaji kweamba mfugaji, Jose, Chui na Kidauya wataondoka lini hapa makazi ya watu tatizo litakwisha siku moja.

Na wala sio shida yetu waondoke kijijini, nchi hii sote wa Tanzania ila whamie maeneo na kuchunga mbali ya makazi ya watu, ng'ombe wasionekane kijijini kabisa. Kila mtu atakuwa na amani.

Nitashukuru sana kama nitasaidiwa kwa hilo sababu pale kijijini wakulima wamekata tamaa na hakuna anaetaka kumfunga paka kengele.
 
Mkuu Wa Wilaya yupo Instagram. Mtumie DM kule.

Poleni sana kwa Changamoto ya Wafugaji.
 
Wafugaji wa mtindo wa ufugaji huria ni jeuri sijawahi kuona, mifugo yao inakula mazao na hata ukienda kwa viongozi, hawawafanyi lolote zaidi ya kuzingua tu.
 
Mkuu Wa Wilaya yupo Instagram. Mtumie DM kule.

Poleni sana kwa Changamoto ya Wafugaji.
OK DM unatumaje rafiki natumia insta ila sijui hiyo DM nielekeze kama hutajali, maana mwenyekiti longolongo sana tulipomwambia akasema nae kashindwa sasa akawa anatuhamasisha wananchi tujikusanye kama maandamano tuwaendee wamang'ati kuwashurutisha wahamme. Hilo jambo mi naona ni hatari wale jamaa wataona wamevamiwa lolote laweza kutokea. Yaan kuna vijiji vingine ujinga mwingi sana
 
Funga safari..mfuate Mkuu was Wiliya ofisini KWAKE...Au andika barua kwa Mkuu wa Wilaya hiyo.ukiwa na viambatanishi vya barua mlizo wapa hao wafugaji na wakaendelea kudharau.
 
Funga safari..mfuate Mkuu was Wiliya ofisini KWAKE...Au andika barua kwa Mkuu wa Wilaya hiyo.ukiwa na viambatanishi vya barua mlizo wapa hao wafugaji na wakaendelea kudharau.
hizo barua huwezi kuzipata mtu sababu inaeleka mmoja wa viongozi wa kijijini hapo na hasa mwenyekiti anakula nao ndio mchezo unaanzia hapo. Yaani mtendaji ndio mtu anaepata mshahara wa serikali wengine wote wakulima au wakata mkaa, akipewa 50 tu au laki kabisa hamgusi mfugaji tena. Hivyo mfuhaji kwao ni fursa.
 
Back
Top Bottom